dc.description.abstract | Katika utafiti huu tumeshughulikia upole kama unavyobainika katika mawasiliano baina ya
wahusika katika tamthilia ya Natala. Tumetumia mtazamo wa nadharia ya Upole ya Brown na
Levinson (1987) na kuzamia katika kipengele cha mikakati ya upole. Data ya uchunguzi huu
ilitokana na matamko ya wahusika katika tamthilia ya Natala. Kauli na matamshi ya wahusika
ziliainishwa kiuana na kubainisha zile zilizotumia mikakati ya upole. Lengo la kwanza lilikuwa
kubainisha ikiwa wahusika wa kiume wanatumia mikakati ya uople katika Natala. Matokeo
yamedhihirisha kuwa wanaume wanatumia mikakati ya upole katika tamthilia ya Natala kuokoa
nyuso za wahusika wanaotagusana nao. Hata hivyo imebainika kuwa matumizi ya mkakati hasi
wa upole ndio mkakati maarufu miongoni mwa wahusika wa kiume katika Natala. Lengo la pili
lilikuwa kuchunguza ikiwa wahusika wa kike wanatumia mikakati ya upole kuwasiliana.
Uchunguzi huu unaonyesha kuwa wanawake hutumia mikakati yote minne ya upole. Hata hivyo
imebainika kuwa wanawake hutumia mkakati chanya wa upole zaidi. Mkakati ndani ya rekodi
kwa upande mwingine unatumiwa kwa njia finyu na wanawake. Aidha tulidhamiria kuonyesha
kuwa mikakati ya upole hufanikisha uwasilishaji wa ujumbe kupitia maudhui. Matokeo
yanaonyesha kuwa maudhui katika tamthilia ya Natala kama ufisadi, taasubi ya kiume, mila na
desturi, umaskini miongoni mwa mengine, yanaibuliwa kupitia matumizi ya mikakati ya upole.
Kijumla ni kuwa, kazi hii imeonyesha kuwa pragmatiki mitindo ni kitengo muhimu katika
uchunguzi wa fasihi. Hii ni kwa sababu msikilizaji lazima awe na umilisi wa kipragmatiki ili
kuelewa maana kamili ya msemaji kwa kuzingatia muktadha wa mazungumzo | en_US |