Show simple item record

dc.contributor.authorNyutu, Wanjiku J
dc.date.accessioned2017-01-09T09:43:27Z
dc.date.available2017-01-09T09:43:27Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/99911
dc.description.abstractKatika tasnifu hii tulichunguza mtindo katika kazi za kubuni za mwandishi Leonard Sanja. Kazi hizi ni “Mimba Ingali Mimba” katika Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine (mh McOnyango) (2006), “Mwavyaji wa Roho” katika Mwavyaji wa Roho na Hadithi Nyingine (mh Sanja) (2011) (hadithi fupi), Zinguo la Mzuka (2011) (tamthilia), Yasinya (2014) (riwaya). Tulitumia nadharia ya Umitindo kuchanganua kazi hizi nne kitaaluma. Tasnifu yetu ina sura tano. Katika sura ya kwanza tulieleza swala la utafiti ambalo lilikuwa kuchunguza mtindo na hasa kipengele cha tamathali za usemi katika kazi nne teule za Sanja. Sababu iliyotupelekea kuchagua mada hii ni kuwa kazi hizi zilichapishwa miaka michache iliyopita na hivyo tuligundua kuwa hakuna ufafiti uliokuwa umefanyiwa kazi hizi nne kimtindo na hasa kipengele cha tamathali za usemi. Tulichunguza tofauti za kimtindo baina ya tanzu tofauti tofauti za fasihi andishi ambapo tuligundua kuwa kila utanzu wa fasihi andishi huwa na wasifu unaoutofautisha na utanzu mwingine katika fasihi andishi. Tulitambua vipengele vya kimtindo na hasa tamathali za usemi katika kazi nne teule za L. Sanja na tuligundua kuwa vipengele tulivyochunguza vya majazi, jazanda, kinaya, kejeli na ndoto zilidhihirisha upekee katika kazi za Sanja. Tulidhibitisha upekee wa kimtindo wa mwandishi Sanja katika kazi zake nne ambao ulidhihirika katika: Hisia zake, usimulizi aliotumia, uteuzi wa msamiati, muundo wa kazi na uchanganyaji wa tamathali mbali mbali. Katika kuchunguza upekee wa mwandishi Sanja tuligundua kuwa alitumia mbinu ya jazanda kwa mapana ili kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira yake. Kazi zake pia zilidhihirisha hisia za kusinyika, kukirihika na kutofurahishwa na tabia za viongozi wa Kiafrika za ufisadi, ubinafsi, kutoshirikiana na pia uongozi mbaya uliowaudhi raia wao.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectMtindo Katika Kazi Za Kubunien_US
dc.titleMtindo Katika Kazi Za Kubuni Za Leonard Sanjaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States