Uhakiki wa usimulizi katika riwaya ya Walenisi ya Katama Mkangi
View/ Open
Date
2005Author
Ong'ondi, Bogonko E
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia uhakiki na unakidi wa riwaya ya Walenisi iliyoandikwa na
marehemuMkangi na kutolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa tisaini na tano (1995).
Kazihii tumeigawa katika sura sita. Katika sura ya kwanza, tumeweka wazi pendekezo la
utafitikwa kuonyesha tatizo la utafiti, sababu za utafiti wenyewe, nadharia tete, msingi
wakinadharia na mbinu za utafiti.
Vilevile tumeshughulikia upeo na mipaka ya utafiti huu miongoni mwa vipengee vingine
vya pendekezo. Sura ya piliinahusu mtazamo kama kipengee mojawapo cha usimulizi.
Katikasura hii tumejadili na kuweka wazi maana ya mtazamo na kuonyesha tofauti baina
ya mtazamo na usimulizi.
Kadhalika, tumeshughulikia sawia mbalimbali za usimulizi katika riwaya ya Walenisi.
Vilevile tumeonyesha aina za usimulizi najinsi zinavyodhihirika katika riwaya hii.
Katika sura ya tatu, tumeshughulikia unenaji na fikira kama kipengee cha usimulizi.
Tumejadili aina tofauti tofauti za unenaji na fikira na kutoa mifano ya kudhihirika kwao
katika riwaya hii.
Nayo sura ya nne, inaangazia wakati kama kipengeekimojawapo cha usimulizi. Katika
sura hii, tumejadili maana ya wakati na umuhimu wake katika usmulizi. Pia tumeonyesha
jinsi mbalimbali wakati hudhihirika katika hadithi.
Katika sura ya tano, tumejadili mpangilio na uwasilishaji kama.kipengee cha usimulizi.
Tumeonyesha wazi kuwa hadithi inaweza kuwa na mpangilio wa moja kwa moja au iwe
na mpangilio changamano ambapo kuna uegemezaji. Katika riwaya hii kuna mtindo
changamano amhapo tumeonyesha na kufafanua ni kwa nini Mkangi akatumia mtindo
huu.
Vile vile, katika sura hii, tumeonyesha jinsi hadithi ya Walenisi imewasilishwa ambapo
kuna mimesia na daigesia kama mbinu za uwasilishaji hadithi.
Tumehitisha katika sura ya sita kwa kurejelea tuliyoyajadili katika sura zote za awali kwa
muhtasari tu. Kadhalika tumeelezea matokeo ya utafiti wetu pamoja na matatizo
tuliyokumbana nayo tukifanya utafiti huu. Hatimaye tumetoa mapendekezo kuhusu
mtalaa huu.
Citation
M.A (Swahili) 2005 ThesisSponsorhip
University of NairobiPublisher
Depatment of Linguistics, University of Nairobi
Description
Master of Arts Thesis