Uhalisiajabu Unavyojitokeza Katika Ukawafi Wa Miiraji Na Utenzi Wa Fumo Liyongo
View/ Open
Date
2016Author
Onchwati, Jared S
Type
ThesisLanguage
OthersMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulikusudia kuonyesha sifa za kiuhalisiajabu uanavyojitokeza katika Utenzi wa Ukawafi wa
Miiraji na Utenzi wa fumo Liyongo. Tulifanya hivyo kwa kuwarejelea baadhi ya wahusika na mandhari
kama yalivyosawiriwa katika tenzi zenyewe. Madhumuni yetu katika utafiti huu yalikuwa kudhihirisha
uhalisiajabu ulivyosawiriwa katika tenzi. Aidha tulibaini kuwa sifa za kiuhalisijabu zilikuwa nguzo
muhimu kwa watunzi wa tenzi hizi katika kufikia malengo yao mbali na wao kutengana kiwakati na
kiumri.
Tulifikia uchanganuzi huu baada ya kutambua kuwa, uhalisiajabu katika tenzi haujatafitiwa sana ilihali
ni mojawapo wa fasihi kongwe zaidi kuliko riwaya na tamthilia. Tumeangalia sifa za takribani wahusika
wote katika tenzi hizi, mazingira walimolelewa pamoja na jamii zilizowazaa na kuwalea. Vilevile
tumeangalia umuhimu wao katika jamii zao. Data ilikusanywa maktabani, mtandaoni na kuchanganuliwa
kwa misingi ya nadharia ya uhalisiajabu iliyoasisiwa na Franz Roh(1925)
Matokea ya utafiti wetu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima wa utafiti wetu.
Kupitia sifa za wahusika na mandhari, tuligundua kuwa tenzi zimeshaheni uhalisiajabu sawia na vipera
vingine vya fasihi. Mbali na tenzi zote mbili kudhihirisha sifa za kiuhalisiajabu, ilidhihirika kuwa
dhamira ya watunzi hawa zilitofautiana mno. Tuligundua kuwa uhalisiajabu husawiriwa vyema katika
mandhari, wahusika wenye sifa za kibinadamu na wale wasiokuwa na sifa za kibinadamu. Aidha
tulibaini kuwa wahusika wa aina hizi zote, ni sehemu muhimu katika kujenga historia ya jamii zao na
dunia yote kwa ujumla.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: