Show simple item record

dc.contributor.authorOnchwati, Jared S
dc.date.accessioned2017-01-10T13:30:30Z
dc.date.available2017-01-10T13:30:30Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/100224
dc.description.abstractUtafiti huu ulikusudia kuonyesha sifa za kiuhalisiajabu uanavyojitokeza katika Utenzi wa Ukawafi wa Miiraji na Utenzi wa fumo Liyongo. Tulifanya hivyo kwa kuwarejelea baadhi ya wahusika na mandhari kama yalivyosawiriwa katika tenzi zenyewe. Madhumuni yetu katika utafiti huu yalikuwa kudhihirisha uhalisiajabu ulivyosawiriwa katika tenzi. Aidha tulibaini kuwa sifa za kiuhalisijabu zilikuwa nguzo muhimu kwa watunzi wa tenzi hizi katika kufikia malengo yao mbali na wao kutengana kiwakati na kiumri. Tulifikia uchanganuzi huu baada ya kutambua kuwa, uhalisiajabu katika tenzi haujatafitiwa sana ilihali ni mojawapo wa fasihi kongwe zaidi kuliko riwaya na tamthilia. Tumeangalia sifa za takribani wahusika wote katika tenzi hizi, mazingira walimolelewa pamoja na jamii zilizowazaa na kuwalea. Vilevile tumeangalia umuhimu wao katika jamii zao. Data ilikusanywa maktabani, mtandaoni na kuchanganuliwa kwa misingi ya nadharia ya uhalisiajabu iliyoasisiwa na Franz Roh(1925) Matokea ya utafiti wetu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima wa utafiti wetu. Kupitia sifa za wahusika na mandhari, tuligundua kuwa tenzi zimeshaheni uhalisiajabu sawia na vipera vingine vya fasihi. Mbali na tenzi zote mbili kudhihirisha sifa za kiuhalisiajabu, ilidhihirika kuwa dhamira ya watunzi hawa zilitofautiana mno. Tuligundua kuwa uhalisiajabu husawiriwa vyema katika mandhari, wahusika wenye sifa za kibinadamu na wale wasiokuwa na sifa za kibinadamu. Aidha tulibaini kuwa wahusika wa aina hizi zote, ni sehemu muhimu katika kujenga historia ya jamii zao na dunia yote kwa ujumla.en_US
dc.language.isoOthersen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUhalisiajabu Unavyojitokeza Katika Ukawafi Wa Miiraji Na Utenzi Wa Fumo Liyongoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States