Show simple item record

dc.contributor.authorChepkorir, Florah
dc.date.accessioned2017-01-12T06:27:46Z
dc.date.available2017-01-12T06:27:46Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/100368
dc.description.abstractTasnifu hii inatoa matokeo ya uchanganuzi wa mtindo katika tahariri ya gazeti la Taifa Leo. Utafiti huu ulinuia kuchanganua uteuzi wa maneno, virai na miundo ya sentensi iliyotumiwa na mwandishi wa tahariri ya Taifa Leo. Pia, uchunguzi wa mbinu za lugha na tamathali za usemi ulifanywa. Tahariri za miezi ya Januari hadi Machi zilikusanywa na kuchunguzwa, kisha tahariri 30 zikateuliwa; zile zilizosheheni mbinu za lugha na tamathali za usemi na mtindo wa pekee katika uteuzi wa maneno. Nadharia ya Umitindo ilitumiwa katika uchunguzi huu. Matokeo ya uchunguzi huo yalibainisha kuwa tamathali za usemi zinazotumika kwa wingi ni tashbihi, misemo/nahau na sitiari, zingine ni kinaya, maswali ya balagha, tashihisi, kwelikinzani na taswira. Pili, matokeo yalibainisha kuwa, mwandishi anateua maneno na virai, anatumia takwimu na miundo ya sentensi inayowasilisha ujumbe unaoonyesha mwelekeo na mtazamo wake. Matokeo pia yalibainisha kuwa mhariri anatumia lugha nyepesi inayoeleweka na wasomaji bila kusababisha utata wowote. Sifa zifuatazo za tahariri ya gazeti la Taifa leo zilidhihirika: mwandishi wa tahariri ya Taifa Leo anatumia mada zinazotoa muhtasari wa ujumbe uliomo, mhariri anaonyesha msimamo wake kuhusu suala linalozungumziwa kwa kuteua maneno kwa njia maalum, tamathali za usemi zinazoeleweka kwa urahisi hutumiwa kupamba lugha, takwimu zinatumika ili kudhihirisha usahihi wa ujumbe, na mwisho mhariri hushughulikia mambo yanayoathiri wanajamii na kusema kwa niaba yao.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUchanganuzi Wa Mtindo Katika Tahariri Ya Gazeti La Taifa Leoen_US
dc.titleUchanganuzi Wa Mtindo Katika Tahariri Ya Gazeti La Taifa Leoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States