Nafasi Ya Aina Za Matini Katika Kushawishi Mbinu Za Tafsiri: Tathmini Ya Mwanzo, Kutoka Na Zaburi Katika Biblia

View/ Open
Date
2017Author
Otwera, Albert, O
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Suala la ulinganifu katika tafsiri si la kiwango cha maneno na sentensi pekee yake. Uelewa wa vipengele vingine vya ulinganifu kama vile aina za matini na rejesta una natija kwa mfasiri kwa kuwa humwezesha kubaini mbinu mwafaka ya kutafsiri matini ya aina fulani anayoishughulikia. Utafiti huu umeshughulikia nafasi ya aina za matini na nduni zake katika kushawishi mbinu za tafsiri kwa kutathmini vitabu vya Mwanzo II, Kutoka 20 na Zaburi 23. Dhana ya aina za matini imefafanuliwa kwa kina. Tumeainisha aina kadha za matini na kuonyesha jinsi ambavyo nduni zake zinavyoshawishi mbinu za tafsiri. Tumeonyesha umuhimu wa upekee na umbo la kila matini na uamilifu wake wa kimawasiliano katika uhawilishaji wa ujumbe wa matini chanzi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: