Mikakati Ya Upole Katika Mstahiki Meya Ya Timothy Arege
View/ Open
Date
2017Author
Endovu, Braicy I
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu umeshughulikia suala la upole kama linavyodhihirishwa katika tamathali za usemi na ukuzaji wa maudhui katika tamthilia ya Mstahiki Meya. Tumetumia mtazamo wa Nadharia ya Brown na Levinson (1987) hasa kipengele cha mikakati ya upole. Data ya utafiti huu ilitokana na uchambuzi wa matamshi ya wahusika katika tamthilia ya Mstahiki Meya. Lengo la kwanza la utafiti huu lilikuwa ni kubainisha iwapo tamathali za usemi hudhihirisha upole katika mazungumzo ya wahusika. Matokeo yanadhihirisha kuwa, tamathali za usemi katika tamthilia ya Mstahiki Meya zimedhihirisha upole kutoka na namna wahusika wanavyoingiliana. Lengo la pili la utafiti huu lilikuwa kubainisha iwapo upole hudhihirika katika ukuzaji wa maudhui katika tamthilia ya Mstahiki Meya. Utafiti huu ulidhamiria pia kuchunguza iwapo miktadha mbalimbali ya mazungumzo huchangia kudhihirisha upole. Matokeo yanaonyesha kuwa, matumizi ya mikakati ya upole hudhihirika kupitia miktadha mbalimbali ya mawasiliano. Kwa jumla, utafiti huu umedhihirisha kuwa, upole una nafasi kubwa katika kuimarisha kazi ya tamthilia. Kwa hivyo, ndiposa mawasiliano yakamilike ni lazima viwango na matumizi ya mikakati ya upole ya wahusika yazingatiwe
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: