Uchanganuzi Wa Kipragmatiki Wa Utoupole Katika Filamu Za Kiswahili
Abstract
Tasnifu hii imeshughulikia suala la utoupole katika filamu nne za Kiswahili kutoka Tanzania ambazo ni Hila, Tabasamu Ghushi, Upepo wa baridi na Majuto ambazo ziliteuliwa kimakusudi ili kutupatia data iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya utafiti huu ilitokana na uchambuzi wa kauli za waigizaji wa filamu husika na kuzichanganua kwa msingi wa nadharia ya utoupole ya Culpeper (1996). Lengo la kwanza la utafiti huu lilikuwa kubainisha na kujadili mikakati ya utoupole katika kauli za waigizaji wa filamu husika. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba mikakati ya utoupole iliyopendekezwa na Culpeper (1996) inatumiwa na waigizaji wa filamu husika kwa lengo la kuhasiri nyuso za waigizaji wenzao. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba mkakati ndani ya rekodi wa utoupole ndio mkakati unaotumiwa zaidi na waigizaji wa filamu husika huku ukirekodi frikwensi ya asilimia 45.2 %, huku mkakati wa kutowasilisha chochote ukiwa mkakati ambao hautumiwi sana kwa kurekodi frikwensi ya asilimia 4.0%. Vilevile, uchunguzi huu ulilenga kuchunguza namna waigizaji wa filamu husika wanakabiliana na hali ya utoupole katika mazungumzo. Matokeo yamebainisha kwamba mbinu ya msikilizaji kujikinga dhidi ya vitendo vinavyohasiri uso ndiyo mbinu inayotumiwa zaidi huku ikirekodi frikwensi ya asilimia 60 %.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: