Show simple item record

dc.contributor.authorNyangi, Lilian, C
dc.date.accessioned2017-12-14T09:45:55Z
dc.date.available2017-12-14T09:45:55Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/101907
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia suala la utoupole katika filamu nne za Kiswahili kutoka Tanzania ambazo ni Hila, Tabasamu Ghushi, Upepo wa baridi na Majuto ambazo ziliteuliwa kimakusudi ili kutupatia data iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya utafiti huu ilitokana na uchambuzi wa kauli za waigizaji wa filamu husika na kuzichanganua kwa msingi wa nadharia ya utoupole ya Culpeper (1996). Lengo la kwanza la utafiti huu lilikuwa kubainisha na kujadili mikakati ya utoupole katika kauli za waigizaji wa filamu husika. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba mikakati ya utoupole iliyopendekezwa na Culpeper (1996) inatumiwa na waigizaji wa filamu husika kwa lengo la kuhasiri nyuso za waigizaji wenzao. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba mkakati ndani ya rekodi wa utoupole ndio mkakati unaotumiwa zaidi na waigizaji wa filamu husika huku ukirekodi frikwensi ya asilimia 45.2 %, huku mkakati wa kutowasilisha chochote ukiwa mkakati ambao hautumiwi sana kwa kurekodi frikwensi ya asilimia 4.0%. Vilevile, uchunguzi huu ulilenga kuchunguza namna waigizaji wa filamu husika wanakabiliana na hali ya utoupole katika mazungumzo. Matokeo yamebainisha kwamba mbinu ya msikilizaji kujikinga dhidi ya vitendo vinavyohasiri uso ndiyo mbinu inayotumiwa zaidi huku ikirekodi frikwensi ya asilimia 60 %.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUchanganuzi Wa Kipragmatiki Wa Utoupole Katika Filamu Za Kiswahilien_US
dc.titleUchanganuzi Wa Kipragmatiki Wa Utoupole Katika Filamu Za Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States