Show simple item record

dc.contributor.authorMuna, Edwin O
dc.date.accessioned2017-12-14T09:57:41Z
dc.date.available2017-12-14T09:57:41Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/101910
dc.description.abstractKatika miaka ya tangu 1970, watafiti mbalimbali wamechunguza uanisho wa lugha za ulimwengu uliofanywa na Talmy (1975, 1985, 2000) kwa kuzingatia vitendo sogezi. Talmy anaeleza kuwa kitendo sogezi kina vipengele vinne vya ndani na lazima na vipengele viwili vya nje na hiari. Anatumia kipengele cha njia kuainisha lugha za ulimwengu katika aina mbili: mfumbatio-tenzi na mfumbatio-kifuatilizi kwa kutegemea kipashio cha kileksia au kisintaksia kinachoeleza kipengele hiki cha kisemantiki. Kumekuwapo na madai kuwa lugha zote za Kiafrika, ikiwamo Kiswahili, ni lugha za mfumbatio-tenzi (Taz. Schaefer & Gaines 1997, Fortis 2010). Hata hivyo, madai haya yametolewa bila utafiti wa kuridhisha kuhusu vitendo sogezi katika Kiswahili. Katika utafiti huu, hivyo basi, nililenga kubainisha uainisho muafaka kwa lugha ya Kiswahili kuhusiana na vitendo sogezi na vipashio vinavyotumika kueleza vipengele vya vitendo sogezi katika lugha hii na vipashio ambavyo huleksisha vipengele vya vitendo sogezi. Ili kufikia malengo haya, nilikusanya data kwa majaribio mawili. Katika Jaribio la 1 washiriki walipewa vitenzi kadha vya usogezi ili wavitungie sentensi. Katika Jaribio la 2 washiriki walipewa kitabu cha picha cha Mayer (1969) na kuombwa kusimulia matukio yaliyomo katika kila ukurasa. Nilichanganua data kwa kuzingatia mawazo ta Talmy aliyoyapendekeza kwa misingi ya nadharia ya Semantiki Tambuzi. Nilibainisha kuwa, ingawa Kiswahili hueleza kipengele cha njia katika vifuatilizi, hupendelea zaidi kuleksisha kipengele hiki katika mizizi ya vitenzi sogezi vyake. Kwa hivyo, Kiswahili ni lugha mfumbatio-tenzi. Vilevile, nilibainisha kuwa Kiswahili hutumia vipashio kama viambishi, maneno, virai na vishazi kueleza vipengele mbalimbali vya vitendo sogezi.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectVitendo Sogezien_US
dc.subjectVitendo Sogezien_US
dc.titleVitendo Sogezi Katika Kiswahili Sanifuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States