Mifichamo Katika Mashairi Ya Mrisho Mpoto: Nikipata Nauli Na Sizonje
View/ Open
Date
2018Author
Nyamboga, Daniel
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulipania kuchunguza mifichamo katika mashiri mawili teule ya Mrisho Mpoto ya Nikipata Nauli na Sizonje. Kwa kutumia maoni ya Grice (1975) kuhusu kanuni za utaratibu wa ushirikiano wa kimazungumzo tuliaangalia jinsi ukiukaji wa kanuni za ukweli, idadi, uhusiano na namna unavyozua mifichamo katika kauli. Tulichunguza mashairi hayo teule ili kutambua kauli zinazokiuka kanuni za utaratibu wa ushirikiano wa kimazungumzo na kuhakiki mifichamo inayojitokeza kwa msikilizaji kutokana na ukiukaji wa kanuni hizo. Aidha tulionyesha namna mfichamo huo unavyochangia katika kukuza maudhui mbali mbali katika mashairi haya mawili. Utafiti huu, unapendekeza kutumia mtazamo wa kipramatiki-mitindo, wa kuhakiki kazi za kisanaa katika kuonyesha namna mtindo wa matumizi ya lugha wa Mrisho Mpoto ulivyochangia katika kuleta ukiukaji wa kanuni katika kauli zake. Aidha tuliangalia mchango wa mkutadha katika ufasiri wa maana za kazi za kifasihi. Kwa kufanya hivyo tuliona namna kanuni au maarifa ya kipragmatiki yalivyotumika kueleza maana katika kazi ya kisanaa, hasa ushairi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: