Makosa Ya Kifonolojia Na Kimofolojia Miongoni Mwa Wanafunzi Wa Kiswahili Wazungumzaji Wa Kikuria Na Wa Kiluo
Abstract
Lugha ya kwanza huathiri ujifunzaji wa lugha ya pili. Kutokana na hali hii wanafunzi wengi wanaojifunza Kiswahili kama lugha yao ya pili, huishia kuhawilisha mfumo wa kiisimu wa lugha yao ya kwanza hadi kwenye Kiswahili. Madhumuni ya utafiti huu ni kuchanganua makosa ya kifonolojia, kimofofonolojia na kimofolojia yanayojitokeza katika kazi za Kiswahili za wanafunzi wazungumzaji wa Kikuria na wa Kiluo. Utafiti huu umeangazia ni kwa kiwango kipi lugha ya kwanza ya wanafunzi huchangia makosa hayo. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, wanafunzi wa darasa la nane kutoka jamii-lugha mbili tofauti walihusishwa. Wanafunzi hawa walishirikishwa katika mijadala ambayo ilirekodiwa kwa kutumia vinasa sauti. Aidha waliandika insha yenye mada, “Siku ambayo sitaisahau maishani”.Data hizo za kimazungumzo na kimaandishi zilichanganuliwa kwa kulenga tu makosa ya kifonolojia, kimofofonolojia na ya kimofolojia. Uchanganuzi wa makosa ya wanafunzi hawa ulifanywa kwa msingi wa kinadharia wa Uchanganuzi Makosa. Makosa hayo yaliainishwa katika viwango vya kifonolojia, kimofofonolojia na kimofolojia kisha kubaini sababu zinazosababisha ukoseaji huo. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa tatizo sugu la uyabisi ni uhawilishaji wa L1 ya wanafunzi hadi LL pamoja na upijinishaji. Yaani Kikuria au Kiluo kama L1 ya wanafunzi hawa kimechangia pakubwa kutokea kwa makosa ya kifonolojia, kimofofonolojia na ya kimofolojia katika utamkaji na uandikaji wao wa Kiswahili sanifu.Utafiti huu ni muhimu kwa watafiti, wakuza mitaala na walimu wa Kiswahili
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: