Show simple item record

dc.contributor.authorMwita, Peter N
dc.date.accessioned2019-01-17T13:25:07Z
dc.date.available2019-01-17T13:25:07Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/105008
dc.description.abstractLugha ya kwanza huathiri ujifunzaji wa lugha ya pili. Kutokana na hali hii wanafunzi wengi wanaojifunza Kiswahili kama lugha yao ya pili, huishia kuhawilisha mfumo wa kiisimu wa lugha yao ya kwanza hadi kwenye Kiswahili. Madhumuni ya utafiti huu ni kuchanganua makosa ya kifonolojia, kimofofonolojia na kimofolojia yanayojitokeza katika kazi za Kiswahili za wanafunzi wazungumzaji wa Kikuria na wa Kiluo. Utafiti huu umeangazia ni kwa kiwango kipi lugha ya kwanza ya wanafunzi huchangia makosa hayo. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, wanafunzi wa darasa la nane kutoka jamii-lugha mbili tofauti walihusishwa. Wanafunzi hawa walishirikishwa katika mijadala ambayo ilirekodiwa kwa kutumia vinasa sauti. Aidha waliandika insha yenye mada, “Siku ambayo sitaisahau maishani”.Data hizo za kimazungumzo na kimaandishi zilichanganuliwa kwa kulenga tu makosa ya kifonolojia, kimofofonolojia na ya kimofolojia. Uchanganuzi wa makosa ya wanafunzi hawa ulifanywa kwa msingi wa kinadharia wa Uchanganuzi Makosa. Makosa hayo yaliainishwa katika viwango vya kifonolojia, kimofofonolojia na kimofolojia kisha kubaini sababu zinazosababisha ukoseaji huo. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa tatizo sugu la uyabisi ni uhawilishaji wa L1 ya wanafunzi hadi LL pamoja na upijinishaji. Yaani Kikuria au Kiluo kama L1 ya wanafunzi hawa kimechangia pakubwa kutokea kwa makosa ya kifonolojia, kimofofonolojia na ya kimofolojia katika utamkaji na uandikaji wao wa Kiswahili sanifu.Utafiti huu ni muhimu kwa watafiti, wakuza mitaala na walimu wa Kiswahilien_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMakosa Ya Kifonolojia Na Kimofolojia Miongoni Mwa Wanafunzi Wa Kiswahili Wazungumzaji Wa Kikuria Na Wa Kiluoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States