Matumizi Ya Tamathali Za Usemi Teule Katika Utenzi Wa Qiyama.
![Thumbnail](/bitstream/handle/11295/105031/ALOO%20RONALD.pdf.jpg?sequence=6&isAllowed=y)
View/ Open
Date
2018Author
Aloo, Ronald O
Type
Technical ReportLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika utafiti huu, tumeshughulikia matumizi ya takriri, tashbihi, sitiari, tashihisi na maswali
ya balagha katika Utenzi wa Qiyama. Utenzi huu ni miongoni mwa tenzi ndefu za kidini na
za jadi za Kiswahili. Utenzi wa Qiyama una beti 338 na unahusu tukio la hukumu baina ya
waumini (Waislamu) na Makafiri (Wakristo) utakaofanywa na Mwenye Enzi Mungu na
malaika wake siku ya mwisho. Utenzi wa Qiyama ulihaririwa katika miaka ya 1972 kwa
mujibu wa dibaji ya mhariri, hata hivyo mtunzi wa utenzi huu hajulikani.Katika utafiti wetu,
tumechunguza Utenzi wa Qiyama, kwa kutumia uhakiki wa kimtindo. Nadharia hii
imetuwezesha kuchunguza kipengele cha tamathali za usemi hasa takriri, tashbihi, sitiari,
tashihisi na maswali ya balagha na tumebainisha kuwa tamathali hizi zimechangia katika
kujenga taswira ya Siku ya Kiyama. Katika utafiti wetu, tumenuia kuonyesha kuwa Utenzi
wa Qiyama una matumizi mengi sana ya takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya
balagha na kuwa tamathali hizi tano ndizo kiini cha taswira ya Siku ya Kiyama katika Utenzi
wa Qiyama. Utafiti wetu umekuwa wa maktabani. Tumesoma mashairi na tenzi nyingi za
kale kwa vile tenzi hizi ndizo zinawekea msingi ushairi wa Kiswahili. Aidha, tumesoma
majarida, makala ya mtandao na vitabu vinavyoeleza dhana za takriri, tashibihi, sitiari,
tashihisi na maswali ya balagha. Tumesoma Utenzi wa Qiyama ili kuelewa matumizi ya
lugha ya utenzi huu. Tumedondoa beti zote ambazo zimetumia mbinu za takriri, tashibihi,
sitiari, tashihisi na maswali ya balagha. Tumeanza kuhakiki utenzi huu bila kujua athari
itakayotokana na takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha katika Utenzi wa
Qiyama. Kisha, tumesoma Utenzi wa Qiyama na kubainisha vile takriri, tashibihi, sitiari,
tashihisi na maswali ya balagha zinavyochangia kwa kukua na kuendelea kwa athari fulani.
Tumetumia maelezo na ufafanuzi wa dhana mbalimbali katika kueleza mchango wa takriri,
tashbihi, tashihisi, sitiari na maswali ya balagha katika ujenzi wa taswira ya Siku ya Kiyama.
Matokeo ya utafiti wetu ni kuwa mtunzi ametumia takriri, tashbihi, sitiari, tashihisi na
maswali ya balagha kwa njia ya kufana na kufikia dhamira yake ya kujenga picha ya Siku ya
Kiyama. Aidha, kwa kutumia tamathali hizi za usemi, mtunzi wa Utenzi wa Qiyama
amefaulu kufikisha ujumbe wake kwa hadhira lengwa huku akitujengea picha halisi ya Siku
ya Kiyama kwa kubana ujumbe huo kwa wasiolengwa, kufikia umbuji wa shairi, kuleta
tasfida, kujenga mshikamano wa kirejelezi, kuleta mshikamano wa kimtindo, kuleta ucheshi,
kuongezea ladha ujumbe kuhusu Siku ya Kiyama, kufafanua na kueleza hisia zake, kuumba
utenzi pamoja na kuboresha kazi yake. Kazi hii imefanikisha uelewa wa tamathali hizi na
utenzi huu pakubwa.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: