Show simple item record

dc.contributor.authorAloo, Ronald O
dc.date.accessioned2019-01-18T05:48:07Z
dc.date.available2019-01-18T05:48:07Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/105031
dc.description.abstractKatika utafiti huu, tumeshughulikia matumizi ya takriri, tashbihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha katika Utenzi wa Qiyama. Utenzi huu ni miongoni mwa tenzi ndefu za kidini na za jadi za Kiswahili. Utenzi wa Qiyama una beti 338 na unahusu tukio la hukumu baina ya waumini (Waislamu) na Makafiri (Wakristo) utakaofanywa na Mwenye Enzi Mungu na malaika wake siku ya mwisho. Utenzi wa Qiyama ulihaririwa katika miaka ya 1972 kwa mujibu wa dibaji ya mhariri, hata hivyo mtunzi wa utenzi huu hajulikani.Katika utafiti wetu, tumechunguza Utenzi wa Qiyama, kwa kutumia uhakiki wa kimtindo. Nadharia hii imetuwezesha kuchunguza kipengele cha tamathali za usemi hasa takriri, tashbihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha na tumebainisha kuwa tamathali hizi zimechangia katika kujenga taswira ya Siku ya Kiyama. Katika utafiti wetu, tumenuia kuonyesha kuwa Utenzi wa Qiyama una matumizi mengi sana ya takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha na kuwa tamathali hizi tano ndizo kiini cha taswira ya Siku ya Kiyama katika Utenzi wa Qiyama. Utafiti wetu umekuwa wa maktabani. Tumesoma mashairi na tenzi nyingi za kale kwa vile tenzi hizi ndizo zinawekea msingi ushairi wa Kiswahili. Aidha, tumesoma majarida, makala ya mtandao na vitabu vinavyoeleza dhana za takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha. Tumesoma Utenzi wa Qiyama ili kuelewa matumizi ya lugha ya utenzi huu. Tumedondoa beti zote ambazo zimetumia mbinu za takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha. Tumeanza kuhakiki utenzi huu bila kujua athari itakayotokana na takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha katika Utenzi wa Qiyama. Kisha, tumesoma Utenzi wa Qiyama na kubainisha vile takriri, tashibihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha zinavyochangia kwa kukua na kuendelea kwa athari fulani. Tumetumia maelezo na ufafanuzi wa dhana mbalimbali katika kueleza mchango wa takriri, tashbihi, tashihisi, sitiari na maswali ya balagha katika ujenzi wa taswira ya Siku ya Kiyama. Matokeo ya utafiti wetu ni kuwa mtunzi ametumia takriri, tashbihi, sitiari, tashihisi na maswali ya balagha kwa njia ya kufana na kufikia dhamira yake ya kujenga picha ya Siku ya Kiyama. Aidha, kwa kutumia tamathali hizi za usemi, mtunzi wa Utenzi wa Qiyama amefaulu kufikisha ujumbe wake kwa hadhira lengwa huku akitujengea picha halisi ya Siku ya Kiyama kwa kubana ujumbe huo kwa wasiolengwa, kufikia umbuji wa shairi, kuleta tasfida, kujenga mshikamano wa kirejelezi, kuleta mshikamano wa kimtindo, kuleta ucheshi, kuongezea ladha ujumbe kuhusu Siku ya Kiyama, kufafanua na kueleza hisia zake, kuumba utenzi pamoja na kuboresha kazi yake. Kazi hii imefanikisha uelewa wa tamathali hizi na utenzi huu pakubwa.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMatumizi Ya Tamathali Za Usemi Teule Katika Utenzi Wa Qiyama.en_US
dc.typeTechnical Reporten_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States