Show simple item record

dc.contributor.authorMugwe, John M
dc.date.accessioned2019-01-21T12:37:33Z
dc.date.available2019-01-21T12:37:33Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/105188
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu uchunguzi wa athari za mtagusano kati ya jamii na ekolojia katika diwani ya Bara Jingine (Mberia, 2001) na Rangi ya Anga (Mberia, 2014). Tumelenga kuchunguza athari za mtagusano baina ya jamii na mazingira. Ili kufaulisha lengo hili tumejikita katika mazingira ya kijiografia kama vile misitu, mito, bahari na kadhalika na kuonyesha jinsi yanavyoathiriwa na mwingiliano baina ya wanajamii. Vilevile tumebainisha jinsi masuala ya kijamii kama vile ufuska, ndoa za mapema, ubaguzi wa kijinsia na teknolojia ya kisasa yanavyoathiri mfumo wa ekolojia jamii. Pia tumebainisha masuala ya kiuchumi na kisiasa kama vile ukosefu wa kazi, ufisadi, uongozi mbaya miongoni mwa mengine yanavyoingiliana na kuathiri mfumo wa ekolojia jamii. Ili kufanikisha haya yote tumeongozwa na Nadharia ya Uhalisia ilioasisiwa na Lukacs mwaka wa 1963. Nadharia hii inadai kuwa msimulizi wa kazi ya fasihi sharti aeleze masuala ya kweli na yanayoweza kuaminika na kuthibitika katika jamii anamoishi. Nadharia hii imetuelekeza katika kubainisha mambo yanayoathiri mfumo wa ekolojia katika hali halisi ya maisha. Pia tumeongozwa na Nadharia ya Mfumo wa Ekolojia ilioasisiwa na Bronfenbrenner mwaka wa 1989. Nadharia hii inadai kuwa maisha ya jamii huathiriwa na watu na viumbe vingine vinayoizunguka. Nadharia hii imetuelekeza katika kubainisha jinsi mahusiano na maingiliano ya jamii yanavyoathiri mfumo wa ekolojia jamii.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleAthari Za Mtagusano Kati Ya Jamii Na Ekolojia Katika Ushairi Wa Kithaka Wa Mberia:bara Jingine Na Rangi Ya Angaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States