Mchango Wa Vijana Wa Kuleta Ukombozi Katika Yasinya, Zinguo La Mzuka Na “mwavyaji Wa Roho”
View/ Open
Date
2018Author
Njeri, Wambui F
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika tasnifu hii tulishughulikia mchango wa vijana katika kuleta ukombozi katika kazi za Leonard Sanja ambazo ni “Mwanyaji wa Roho” katika diwani ya Mwavyaji wa Roho na hadithi Nyingine (2011) Zinguo la Mzuka (2011) na Yasinya (2012). Tulitumia Nadharia ya Uhalisia kuchanganua kazi hizi tatu. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza nafasi ya vijana katika kuleta ukombozi katika kazi hizi tatu na pia kuonyesha changamoto ambazo vijana wanakubana nazo katika kuleta ukombozi. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani ambapo mtafiti alisoma kazi zilizoteuliwa pamoja na vitabu vingine vilivyohusiana na utafiti wetu ili kupata data iliyohitajika. Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti pamoja na nadharia ya uhalisia. Uchanganuzi ulifanywa kwa njia ya maelezo.Utafiti huu ulibaini kuwa vijana wamepewa nafasi kubwa ya kupigania haki za wanaodhulumiwa ili kuleta ukombozi. Ni katika kuungana kwa vijana hawa ambapo walifaulu kuleta ukombozi katika kazi hizi tatu. Hata hivyo, vijana hawa wamekumbwa na matatizo si haba katika juhudi zao za kuleta ukombozi.Licha ya changamoto hizi, utafiti wetu ulibaini kuwa wahusika vijana katika kazi hizi tatu wametoa mchango mkubwa katika juhudi za ukombozi wa jamii zao.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: