Show simple item record

dc.contributor.authorNjeri, Wambui F
dc.date.accessioned2019-01-23T13:33:20Z
dc.date.available2019-01-23T13:33:20Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/105367
dc.description.abstractKatika tasnifu hii tulishughulikia mchango wa vijana katika kuleta ukombozi katika kazi za Leonard Sanja ambazo ni “Mwanyaji wa Roho” katika diwani ya Mwavyaji wa Roho na hadithi Nyingine (2011) Zinguo la Mzuka (2011) na Yasinya (2012). Tulitumia Nadharia ya Uhalisia kuchanganua kazi hizi tatu. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza nafasi ya vijana katika kuleta ukombozi katika kazi hizi tatu na pia kuonyesha changamoto ambazo vijana wanakubana nazo katika kuleta ukombozi. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani ambapo mtafiti alisoma kazi zilizoteuliwa pamoja na vitabu vingine vilivyohusiana na utafiti wetu ili kupata data iliyohitajika. Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti pamoja na nadharia ya uhalisia. Uchanganuzi ulifanywa kwa njia ya maelezo.Utafiti huu ulibaini kuwa vijana wamepewa nafasi kubwa ya kupigania haki za wanaodhulumiwa ili kuleta ukombozi. Ni katika kuungana kwa vijana hawa ambapo walifaulu kuleta ukombozi katika kazi hizi tatu. Hata hivyo, vijana hawa wamekumbwa na matatizo si haba katika juhudi zao za kuleta ukombozi.Licha ya changamoto hizi, utafiti wetu ulibaini kuwa wahusika vijana katika kazi hizi tatu wametoa mchango mkubwa katika juhudi za ukombozi wa jamii zao.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMchango Wa Vijana Wa Kuleta Ukombozi Katika Yasinya, Zinguo La Mzuka Na “mwavyaji Wa Roho”en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States