Matumizi Ya Taswira Katika Tamthilia Za Said Ahmed Mohamed: Pungwa, Kivuli Kinaishi Na Mashetani Wamerudi
View/ Open
Date
2018Author
Nzilu, Muinde D
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Mada ya utafiti huu ilikuwa kuchunguza matumizi ya taswira katika tamthilia za Pungwa, Kivuli Kinaishi na Mashetani Wamerudi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza matumizi ya taswira katika tamthilia hizi na kuonyesha dhamira na athari zinazotokana na taswira zenyewe. Utafiti huu ulinuia kujibu maswali yafuatayo: Je, ni aina gani za taswira anazotumia S.A Mohamed katika tamthilia za Pungwa, Kivuli Kinaishi na Mashetani Wamerudi, Matumizi ya taswira yana athari gani katika tamthilia teule na Je, ni dhamira zipi zinazotokana na matumizi ya tawsira katika tamthilia teule. Nadharia ya umitindo iliyotumiwa katika utafiti huu ilituwekea msingi imara wa kutathmini matumizi ya taswira kama mbinu iliyotumiwa na S.A. Mohamed kuwasilishia maudhui mazito katika tamthilia zake. Kupitia kwa matumizi mufti ya taswira maswala yanayohusu jamii kama vile siasa, uchumi, uozo katika jamii, uongozi mbaya, elimu na mengine mengi yamejadiliwa. Matokeo ya utafiti huu yamethibitishwa kuwa katika sanaa ya uandishi kipengee mahsusi cha lugha kinaweza kutumiwa kama kigezo cha kuainisha kazi za mtunzi binafsi. Mapendekezo yametolewa kuhusu maeneo mengine yanayoweza kufanyiwa utafiti.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: