Taswira ya mwanamke katika tamthilia mbili za Kiswahili
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia taswira ya mwanamke katika tamthilia mbili za Kiswahili. Tumeangalia picha ambayo mwanamke amepewa na jamii katika tamthilia za Kilio Cha Haki (1981) na Pango(2003). Katika sura ya kwanza tumeshughulikia tatizo la utafiti,madhumuni ya utafit,nadharia tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa juu ya mada na njia za utafiti. Katika sura ya pili tumeshughulikia taswira hasi na chanya aliyopewa mwanamke na jamii katika tamthilia ya Kilio cha Haki (1981) Alamin Mazrui na kisha tukaangazia njia ambazo mwanamkeanaweza kuzitumia ili kujikomboa. Sura ya tatu imeshughulikia taswira chanya na hasi aliyopewa mwanamke na jamn katika tamthilia ya Pango (2003) Wamitila K.W na vilevile tukaonyesha njia ambazo mwanamke anaweza kutumia ili kujikomboa. Sura ya nne imeshughulikia hitimisho la utafiti wetu pamoja na mapendekezo.
Publisher
University of Nairobi, Kenya