Uswari wa wahusika wa kike katika tamthilia za Natala na Mama Ee
Abstract
Utafiti huu ulishugulikia usawini wa wahusika wa kike katika tamthilia za natal a na Mama ee kwa kutumia nadharia ya ufeministi. Madhumuni ua utafiti huu yalikuwa; Kuchunguza jinsi watunzi walivyowasawiri wahusika wa kike katika tamthilia za Natala (2011) na Mama ee (2011), Kuchunguza matumizi ya lugha baina na kati ya wahusika katika tamthilia za Natala (2011) na Mama ee (2011), Kuchunguza mandhari ya usimulizi na usimulizi wenyewe katika tamthilia za Natala (2011) na Mama ee (2011). Katika sura ya kwanza tulielezea kwa ufupi maswala ya kimsingi katika utafiti. Tulieleza tatizo letu la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Katika sura hii pia tulishugulikia sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, misingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na njia ya utafiti. Tulitumia mbinu ye maktabani katika kukusanya data tuliohitaji na kuichanganua. Katita sura ya pili tulishugulikia vipengele vya fani katika tamthilia. Katika sura ya taro tulushughulikia ubabedume na historia yake. Katika sura ya nne nayo tulishughulikia wahusika wa kike katika tamthilia ya Mama ee na sura ya tano tukachunguza wahusika wa kike katika tamthilia ya Natala. Katika sura ya sita tulishughulikia muhtasari wa utafiti na mapendekezo ya utafiti.
Publisher
University of Nairobi, Kenya