Show simple item record

dc.contributor.authorMukhata, Chrispinus, W
dc.date.accessioned2021-08-10T07:54:12Z
dc.date.available2021-08-10T07:54:12Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155120
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu uhakiki wa riwaya ya Nyuso za mwanamke (2010) ya Saidi Ahmed Mohamed kwa mtazamo wa saikolojia changanuzi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha, kuchanganua na kubainisha mitagusano inayoibuka katika jamii iliyosawiriwa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke na athari zake kwa wahusika. IIi kuthibitisha hili tulilenga kubainisha mbinu za usukaji wa matukio yenye mwelekeo wa kisaikolojia. Pia, tulidhamiria kuonyesha jinsi mwandishi alikusudia kuwasawiri wahusika ili kudokez.a msukumo wa matendo yao na hall zao 7~ kisaikolojia. Aidha, tulilenga kuonyesha riwaya hii kama riwaya ya kisaikolojia mbali na kubainisba maendelelo ya riwaya ya kisaikolojia katika kitengo cha kimaudhui, kiutanzu, kihusika, kimsuko na kimtindo. Madhumuni haya yote yalidhamiria kuchangia uelewa wa kazi za kifasihi hususani riwaya ya Kiswahili kwa ujumla wake. Katika utafiti wetu tuliongozwa na nadharia tete tatu. Kwanza, tulitaka kubainisha kama riwaya ya NYU.fO Zil Mwann.mke inaweza kuainishwa kama riwaya ya kisaikolojia Pili, kama riwaya ya Nyuso za Mwanamke inaonyesha ukamilifu katika kipengele cha umbuji wa wahusika kati ya vipengele vingine vya riwaya ya kisaikolojia Na tatu, kama mtindo si nyenzo kuu ya kuiunda kisanii riwaya ya Nyuso za mwanamke kama riwaya ya kisaikolojia. Kati ya nadharia tete hizi tatu nadharia mbili za mwanzo zilitimilika vizuri huku tukipata kuwa mtindo ni nyenzo kuu katika kuiunda riwaya hii kisanii kama kazi ya kisaikolojia. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani. Tulidurusu riwaya husika na kazi nyingine za wataalamu wa fasihi hasa fasihi ya Kiswahili kwa undani. Pia, tulirejelea riwaya nyingine za kisaikolojia za Kiswahili ili tupate wasifu wa riwaya ya kisaikolojia vizuri. Kwa maoni yetu, ingekuwa vyema kama utafiti huu ungehusisha udurusu wa shajara za mwandishi huyu pamoja na kuwahoji watu walio karibu naye ili kujua maisha yake. Kufanya hivi kungetuwezesha kuchanganua saikolojia yake ipasavyo. Katika utafiti huu nadharia ya saikolojia changanuzi ilitufaa sana. Ilitufaa katika uchanganuzi wa muundo na wasifu wa ploti, umbuji wa wahusika na mtindo wa usanii wa kazi husika. Ilitufaa pia kuonyesha maudhui kama motifu inayojitokeza katika kazi hii na kazi zake za awali pamoja na kuonyesha kuwa maudhui haya ni akisi ya uhalisi ulio dhahiri katika jamii iliyosawiriwa. Hata hivyo, nadharia hii inajikita sana katika kusawiri hali za kisaikolojia za wahusika na mwandishi na kwa hivyo inawafanya waonekane kama watu walio na matatizo ya kisaikolojia, Mbali na hayo, inao udhaifu wa kuiona kazi ya kifasihi kama ndoto na kwa maana hiyo huenda wasomaji wakaichukulia hivyo na kuipuzilia mbali kama isiyo na mashiko na uhalisi. Mbali na kuwa riwaya ya kisaikolojia haina historia ndefu imeonyesha ukuaji mkubwa sana. Kwa maoni yetu kilele cha ukuaji huo ni riwaya ya Nyuso za Mwanamke: Kwanza, rnatukio katika riwaya hii yamesukwa kwa ufundi mkubwa na uchangarnano kwa mbinu za kisaikolojia kwa lengo la kuonyesha uhusiano kati ya matukio hayo na hali za kisaikolojia za wahusika Mbinu hizi ni kama uzungurnzinafsi ndani, dayolojia ya ndani, mkondo wa ung' amuzi, mbinu rejeshi, barua, ndoto na nyimbo. Wahusika wengi wamesawiriwa kisaikolojia kwa lengo la kudokeza hali zoo za ndani na wanaonyesha mwelekeo mkubwa wa ubanaji, uhawilisho, uhusishi na ubadilishaji kama inavyojitokeza katika wahusika Nana, Faisal na Bimkubwa. Maudhui yamejitokeza kama motifu katika kazi hii na kazi za awali pamoja na kuwa akisi ya uhalisi katika jamii husika. Mtindo umeturnika kwa ufundi mkubwa katika vipengele vyote vya fani. Uhusika umewadokeza wahusika kisitiari na kiishara kama inavyoonekana katika wahusika Nana, Bimkubwa na Faisal. Lugha ya kitamathali imetumika kwa upana sana hasa maswali ya balagha, tasifida, ritifaa, taashira na ishara kwa uamilifu mkubwa wa kisaikolojia na kuchangia kukuza wasifu wa wahusika na maudhui. Mbinu za uwasilishaji mawazo, usimulizi, italiki na sintaksia yenye nyufa zinajitokeza kwa uwazi. Mwisho, tumeiona riwaya hii kuwa ya kuvutia na kusisimua na yenye uchangamano pamoja na kule kuweza kuibua masuala tata na nyeti katika jamii husika Kupitia uchanganuzi wake, tumepata kuwa riwaya ya kisaikolojia ni riwaya ya kipekee katika taaluma ya fasihi. Upekee huu umejitokeza katika usawiri wa wahusika kisaikolojia kwa kutoa mawazo, fikira na hisia za ndani za wahusika, Riwaya hii pia imetumia mbinu tendati zinazoifanya iwe na miondoko ya tamthilia kama uzungumzinafsi ndani, dayolojia ya ndani, uwasilishaji halisi wa mawazo, uwasilishaji halisi huru wa mawazo na mkondo wa ung'amuzi. Kwa njia hii inaweza kunasa raghba ya msomaji yeyote.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUhakiki wa Riwaya ya nyuso za mwanamke na Said Ahmed Mohamed: mtazamo wa saikolojia changanuzien_US
dc.titleUhakiki wa Riwaya ya nyuso za mwanamke na Said Ahmed Mohamed: mtazamo wa saikolojia changanuzien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States