Uhakiki wa Riwaya ya nyuso za mwanamke na Said Ahmed Mohamed: mtazamo wa saikolojia changanuzi
View/ Open
Date
2011Author
Mukhata, Chrispinus, W
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii inahusu uhakiki wa riwaya ya Nyuso za mwanamke (2010) ya Saidi Ahmed Mohamed
kwa mtazamo wa saikolojia changanuzi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha,
kuchanganua na kubainisha mitagusano inayoibuka katika jamii iliyosawiriwa katika riwaya ya
Nyuso za Mwanamke na athari zake kwa wahusika. IIi kuthibitisha hili tulilenga kubainisha mbinu
za usukaji wa matukio yenye mwelekeo wa kisaikolojia. Pia, tulidhamiria kuonyesha jinsi
mwandishi alikusudia kuwasawiri wahusika ili kudokez.a msukumo wa matendo yao na hall zao 7~
kisaikolojia. Aidha, tulilenga kuonyesha riwaya hii kama riwaya ya kisaikolojia mbali na
kubainisba maendelelo ya riwaya ya kisaikolojia katika kitengo cha kimaudhui, kiutanzu, kihusika,
kimsuko na kimtindo. Madhumuni haya yote yalidhamiria kuchangia uelewa wa kazi za kifasihi
hususani riwaya ya Kiswahili kwa ujumla wake.
Katika utafiti wetu tuliongozwa na nadharia tete tatu. Kwanza, tulitaka kubainisha kama riwaya
ya NYU.fO Zil Mwann.mke inaweza kuainishwa kama riwaya ya kisaikolojia Pili, kama riwaya ya
Nyuso za Mwanamke inaonyesha ukamilifu katika kipengele cha umbuji wa wahusika kati
ya vipengele vingine vya riwaya ya kisaikolojia Na tatu, kama mtindo si nyenzo kuu ya kuiunda
kisanii riwaya ya Nyuso za mwanamke kama riwaya ya kisaikolojia. Kati ya nadharia tete hizi tatu
nadharia mbili za mwanzo zilitimilika vizuri huku tukipata kuwa mtindo ni nyenzo kuu katika
kuiunda riwaya hii kisanii kama kazi ya kisaikolojia.
Utafiti huu ulikuwa wa maktabani. Tulidurusu riwaya husika na kazi nyingine za wataalamu wa
fasihi hasa fasihi ya Kiswahili kwa undani. Pia, tulirejelea riwaya nyingine za kisaikolojia za
Kiswahili ili tupate wasifu wa riwaya ya kisaikolojia vizuri. Kwa maoni yetu, ingekuwa vyema
kama utafiti huu ungehusisha udurusu wa shajara za mwandishi huyu pamoja na kuwahoji watu
walio karibu naye ili kujua maisha yake. Kufanya hivi kungetuwezesha kuchanganua saikolojia
yake ipasavyo.
Katika utafiti huu nadharia ya saikolojia changanuzi ilitufaa sana. Ilitufaa katika uchanganuzi wa
muundo na wasifu wa ploti, umbuji wa wahusika na mtindo wa usanii wa kazi husika. Ilitufaa pia
kuonyesha maudhui kama motifu inayojitokeza katika kazi hii na kazi zake za awali pamoja na
kuonyesha kuwa maudhui haya ni akisi ya uhalisi ulio dhahiri katika jamii iliyosawiriwa. Hata
hivyo, nadharia hii inajikita sana katika kusawiri hali za kisaikolojia za wahusika na mwandishi na
kwa hivyo inawafanya waonekane kama watu walio na matatizo ya kisaikolojia, Mbali na hayo,
inao udhaifu wa kuiona kazi ya kifasihi kama ndoto na kwa maana hiyo huenda wasomaji
wakaichukulia hivyo na kuipuzilia mbali kama isiyo na mashiko na uhalisi.
Mbali na kuwa riwaya ya kisaikolojia haina historia ndefu imeonyesha ukuaji mkubwa sana. Kwa
maoni yetu kilele cha ukuaji huo ni riwaya ya Nyuso za Mwanamke: Kwanza, rnatukio katika
riwaya hii yamesukwa kwa ufundi mkubwa na uchangarnano kwa mbinu za kisaikolojia kwa lengo
la kuonyesha uhusiano kati ya matukio hayo na hali za kisaikolojia za wahusika Mbinu hizi ni
kama uzungurnzinafsi ndani, dayolojia ya ndani, mkondo wa ung' amuzi, mbinu rejeshi, barua,
ndoto na nyimbo. Wahusika wengi wamesawiriwa kisaikolojia kwa lengo la kudokeza hali zoo za
ndani na wanaonyesha mwelekeo mkubwa wa ubanaji, uhawilisho, uhusishi na ubadilishaji kama
inavyojitokeza katika wahusika Nana, Faisal na Bimkubwa. Maudhui yamejitokeza kama motifu
katika kazi hii na kazi za awali pamoja na kuwa akisi ya uhalisi katika jamii husika. Mtindo
umeturnika kwa ufundi mkubwa katika vipengele vyote vya fani. Uhusika umewadokeza wahusika
kisitiari na kiishara kama inavyoonekana katika wahusika Nana, Bimkubwa na Faisal. Lugha ya
kitamathali imetumika kwa upana sana hasa maswali ya balagha, tasifida, ritifaa, taashira na ishara
kwa uamilifu mkubwa wa kisaikolojia na kuchangia kukuza wasifu wa wahusika na maudhui.
Mbinu za uwasilishaji mawazo, usimulizi, italiki na sintaksia yenye nyufa zinajitokeza kwa uwazi.
Mwisho, tumeiona riwaya hii kuwa ya kuvutia na kusisimua na yenye uchangamano pamoja na
kule kuweza kuibua masuala tata na nyeti katika jamii husika Kupitia uchanganuzi wake, tumepata
kuwa riwaya ya kisaikolojia ni riwaya ya kipekee katika taaluma ya fasihi. Upekee huu
umejitokeza katika usawiri wa wahusika kisaikolojia kwa kutoa mawazo, fikira na hisia za ndani za
wahusika, Riwaya hii pia imetumia mbinu tendati zinazoifanya iwe na miondoko ya tamthilia kama
uzungumzinafsi ndani, dayolojia ya ndani, uwasilishaji halisi wa mawazo, uwasilishaji halisi huru
wa mawazo na mkondo wa ung'amuzi. Kwa njia hii inaweza kunasa raghba ya msomaji yeyote.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Uhakiki wa Riwaya ya nyuso za mwanamke na Said Ahmed Mohamed: mtazamo wa saikolojia changanuziRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: