Dhana Ya Maisha Katika Riwaya Mbili Za Euphrase Kezilahabi: Kichwamaji Na Dunia Uwanja Wa Fujo
View/ Open
Date
2011Author
Mwanjala, Simion M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika tasnifu hii tumechunguza dhana ya maisha katika nwaya mbili za Euphrase
Kezilahabi ambazo ni Kichwamaji na Dunia Uwanja wa Fujo.
Uhakiki huu umegawanywa katika sura nne. Katika sura ya kwanza tumebainisha somo
la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua somo, upeo na mipaka ya somo,
nadharia tete, yaliyoandikwa kuhusu somo hili, msingi wa kinadharia na njia za utafiti.
Katika sura ya pili, tumeonyesha dhana ya maisha katika riwaya ya Kichwamaji.
Tumevihakiki vipengele/mihimili ya udhanaishi katika riwaya hii,vikiwemo ukengeushi,
kutawala kwa suala la uteuzi na wingi wa uteuzi, fujo katika maisha, udhaifu wa maisha
ya mwanadamu, upweke na usiri, kihoro na hofu kubwa, utupu na ubwege wa maisha,
swala la uhuru, swala la kifo (mauti).
Katika sura ya tatu, tumeonyesha dhana ya maisha katika Riwaya ya Dunia Uwanja wa
Fujo. Vilevile, tumevihakiki vipengele/mihimili ya udhanaishi katika riwaya hii.
Katika sura ya nne, tumehitimisha kwa kutoa maoni yetu kuhusiana na kazi hii kwa
ujumla. Aidha tumetoa maelezo kuhusu mafanikio pamoja na mapendekezo ya utafiti
zaidi.
Tumehitimisha kwa kuonyesha mareje1eo ya baadhi ya kazi ambazo zimeandikwa kuhusu
kazi za Euphrase Kezilahabi na nadharia ya udhanaishi tunazozishughulikia.
Publisher
university of Nairobi
Subject
Dhana Ya Maisha Katika RiwayaRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: