Upembezwaji Wa Mwanamke Kama Udokezi Wa Nafasi Ya Mwanamke Katika Utenzi Wa Fatuma
View/ Open
Date
2011Author
Maina, Hannington G
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia upembezwaji wa mwanamke kama udokezi wa nafasi ya
mwanamke katika Utenzi wa Fatuma.
Kazi imegawika katika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumeshughulikia maswala ya
kimsingi yanayojenga utafiti wetu kama vile: kutambulisha utafiti, sababu ya kuchagua mada,
tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, malengo ya utafiti, msingi wa
kinadharia, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu maada yetu na njia za utafiti tulizotumia.
Katika sura ya pili, tumeshughulikia ubabedumne kama mhimili mkuu wa upembezwaji wa
mwanarnke. Tumeeleza historia ya ubadume kwa kuwa historia hii inatusaidia kuelewa
mfumo wa ubabedume. Baada ya kueleza historia hii, tumezieleza asasi zinazochangia
kuuendeleza mfumo wa ubabedume. Asasi hizi tumezitajakuwa: dini, ndoa, utamaduni na
elimu.
Katika sura ya tatu, tumeuhakiki Utenzi wa Fatuma kwa kutumia nadharia ya ufeministi wa
kirasimi. Tumethibitisha kuwa asasi za ndoa, dini, na utamaduni ndizo zinazochangia
kepembezwa kwa mwanamke katika Utenzi wa Fatuma.
Katika sura ya nne, tumeonyeshajinsi lugha inachangia kupembezwa kwa mwanamke katika
Utenzi wa Fatuma. Mbinu za lugha tulizozieleza ni ishara na uashiriaji na vilevile mbinu ya
sitiari.
Tumetoa mahitimisho yetu katika sura ya tano.
Publisher
university of Nairobi
Subject
Nafasi Ya MwanamkRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: