Show simple item record

dc.contributor.authorKing'ora, Mary N
dc.date.accessioned2021-09-07T07:59:26Z
dc.date.available2021-09-07T07:59:26Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155437
dc.description.abstractUtafiti huu umeongozwa na nadharia ya utendaji iliyoasisiwa na Wallace Bacon ili kubainisha ikiwa tamthilia za Sudana na Kimya Kimya Kimya zimezingatia kigezo kikuu katika matini za kidrama ambacho ni uwezo wa kuwasilishwa jukwaani au ni majibizano ya usemi tu. Katika utafiti huu tumevitathmini vipengele vinavyochochea na kufanikisha utendaji wa tamthilia kwenye jukwaa. Maelekezo ya jukwaa, mandhari, maleba, miondoko, sauti, uangazaji, kimya na mihimili ni vipengele vya utendaji ambavyo huwawezesha waigizaji kuwasilisha ujumbe wa mwandishi kwenye jukwaa. Katika utafiti wetu tumebainisha jinsi vipengele hivi vinavyofanikisha uwasilishaji wa ujumbe kwenye jukwaa na pia kuutaja kwa ufupi ujumbe unaofungamana na vipengele hivi. Tumevichunguza vipengele hivi katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Mohamed (2011) na katika tamthilia ya Sudana ya Mazrui na Njogu (2006). Utafiti huu umeanza kwa somo la utafiti, kisha ufafanuzi wa vipengele vya utendaji. Pia tumevitathmini vipengele vya utendaji katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya. Aidha tumevitathmini vipengele vya utendaji katika tamthilia ya Sudana.Tamati ya utafiti wenyewe inahusu muhtasari wa matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo.
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUtendaji Katika Tamthilia Za Sudana Na, kimya Kimya Kimyaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States