Utendaji Katika Tamthilia Za Sudana Na, kimya Kimya Kimya
View/ Open
Date
2014Author
King'ora, Mary N
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya utendaji iliyoasisiwa na Wallace Bacon ili kubainisha ikiwa tamthilia za Sudana na Kimya Kimya Kimya zimezingatia kigezo kikuu katika matini za kidrama ambacho ni uwezo wa kuwasilishwa jukwaani au ni majibizano ya usemi tu. Katika utafiti huu tumevitathmini vipengele vinavyochochea na kufanikisha utendaji wa tamthilia kwenye jukwaa. Maelekezo ya jukwaa, mandhari, maleba, miondoko, sauti, uangazaji, kimya na mihimili ni vipengele vya utendaji ambavyo huwawezesha waigizaji kuwasilisha ujumbe wa mwandishi kwenye jukwaa. Katika utafiti wetu tumebainisha jinsi vipengele hivi vinavyofanikisha uwasilishaji wa ujumbe kwenye jukwaa na pia kuutaja kwa ufupi ujumbe unaofungamana na vipengele hivi. Tumevichunguza vipengele hivi katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Mohamed (2011) na katika tamthilia ya Sudana ya Mazrui na Njogu (2006). Utafiti huu umeanza kwa somo la utafiti, kisha ufafanuzi wa vipengele vya utendaji. Pia tumevitathmini vipengele vya utendaji katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya. Aidha tumevitathmini vipengele vya utendaji katika tamthilia ya Sudana.Tamati ya utafiti wenyewe inahusu muhtasari wa matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: