Show simple item record

dc.contributor.authorLokidor, Edward L
dc.date.accessioned2021-09-07T08:40:05Z
dc.date.available2021-09-07T08:40:05Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155438
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu mofofonolojia ya nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili ambapo tumechanganua mifanyiko ya kimofofonolojia ambayo nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili hupitia ndipo zikubalike katika Kiturkana. Utafiti huu ulikusudia kuchunguza vipengele vya fonolojia ya Kiturkana kama vile irabu, nusuirabu, konsonanti na silabi. Utafiti huu pia ulilenga kubainisha mabadiliko ya sauti yanayokumba konsonanti na irabu za nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili. Nadharia ya fonolojia zalishi asilia ilielekeza utafiti huu katika kubaini mifanyiko ya kimofofonolojia ambayo nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili hupitia na kanuni zinazodhibiti mifanyiko hii. Tulikusanya data yetu maktabani yaani kutoka kwa Bibilia ya Kiturkana, Misali na Kamusi ya Kiingereza - Kiturkana na kuwasilisha kifonetiki na kiothografia. Utafiti huu umebaini kwamba kuna fonimu ambazo zipo katika Kiswahili lakini hazipo katika Kiturkana. Utafiti huu pia umetambua kwamba konsonanti za Kiswahili zinapokopwa na Kiturkana hupitia mabadiliko ya kifonolojia kama vile udhoofikaji, uimarikaji, udondoshaji, uchopekaji, usilimisho pamwe wa nazali na ubadala wa konsonanti ili nomino hizi zikubalike •katika Kiturkana kwa lengo la kusahilisha utamkaji, kupata muundo mwafaka wa silabi na mofu ya jinsia ambayo hutumiwa kuainisha nomino za Kiturkana. Aidha, tumebaini kwamba vokali za nomino za Kiswahili zinapokopwa na Kiturkana hupitia mabadiliko ya kifonolojia kama vile udondoshaji wa irabu, uchopekaji wa irabu, ubadala wa irabu, uyeyushaji na uwiano wa irabu ili nomino za Kiswahili zikubalike katika Kiturkana ili kusahihilisha utamkaji, upatakaji wa miundo ya silabi na mofu ya nomino husika katika Kiturkana.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMofofonolojia Ya Nomino Mkopo Za Kiturkana Kutoka Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States