Mofofonolojia Ya Nomino Mkopo Za Kiturkana Kutoka Kiswahili
Abstract
Utafiti huu unahusu mofofonolojia ya nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili
ambapo tumechanganua mifanyiko ya kimofofonolojia ambayo nomino mkopo za
Kiturkana kutoka Kiswahili hupitia ndipo zikubalike katika Kiturkana. Utafiti huu
ulikusudia kuchunguza vipengele vya fonolojia ya Kiturkana kama vile irabu, nusuirabu,
konsonanti na silabi. Utafiti huu pia ulilenga kubainisha mabadiliko ya sauti
yanayokumba konsonanti na irabu za nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili.
Nadharia ya fonolojia zalishi asilia ilielekeza utafiti huu katika kubaini mifanyiko ya
kimofofonolojia ambayo nomino mkopo za Kiturkana kutoka Kiswahili hupitia na kanuni
zinazodhibiti mifanyiko hii. Tulikusanya data yetu maktabani yaani kutoka kwa Bibilia
ya Kiturkana, Misali na Kamusi ya Kiingereza - Kiturkana na kuwasilisha kifonetiki na
kiothografia. Utafiti huu umebaini kwamba kuna fonimu ambazo zipo katika Kiswahili
lakini hazipo katika Kiturkana. Utafiti huu pia umetambua kwamba konsonanti za
Kiswahili zinapokopwa na Kiturkana hupitia mabadiliko ya kifonolojia kama vile
udhoofikaji, uimarikaji, udondoshaji, uchopekaji, usilimisho pamwe wa nazali na ubadala
wa konsonanti ili nomino hizi zikubalike •katika Kiturkana kwa lengo la kusahilisha
utamkaji, kupata muundo mwafaka wa silabi na mofu ya jinsia ambayo hutumiwa
kuainisha nomino za Kiturkana. Aidha, tumebaini kwamba vokali za nomino za
Kiswahili zinapokopwa na Kiturkana hupitia mabadiliko ya kifonolojia kama vile
udondoshaji wa irabu, uchopekaji wa irabu, ubadala wa irabu, uyeyushaji na uwiano wa
irabu ili nomino za Kiswahili zikubalike katika Kiturkana ili kusahihilisha utamkaji,
upatakaji wa miundo ya silabi na mofu ya nomino husika katika Kiturkana.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: