Maudhui Yanavyo Imarishwa Na Fani Katika Riwaya Ya Nguvu Ya Sala Ya K.W Wamitila
Abstract
Kazi yetu imechunguza vipengele vya fani. Tulifafanua dhana ya fani kwa kusema kuwa, fani ni
vipengele vya kisanaa katika kazi ya fasihi. Aidha, fani ni jinsi ambavyo msanii hufinyanga kazi
yake ili msomaji apate ujumbe wake kwa njia iliyo nzuri. Kazi yetu imetumia nadharia ya umuundo
kuchambua vipengele vya fani. Kazi hii imechunguza vipengele vifuatavyo; Msuko, mandhari na
wahusika. Tumechunguza namna mandhari mbalimbali yanavyowaathiri wahusika na kubadilisha
misimamo yao kuhusu mambo tofauti.Pia tumechunguza namna mwandishi aliyoendeleza maudhui
yake kwa kutumia misuko ya aina mbali mbali. Aidha tumechunguza namna wahusika tofauti
walivyotumiwa kukuza maudhui ya kazi hii. Kutokana na uchuguzi huu imebainika kuwa maudhui
huimarishwa na mwandishi anapotumia vipengele tofauti vya fani kwa ustadi ili kukuza ujumbe
wake. Hii ni kutokana na kweli kwamba mambo ambayo huelezwa kikawaida hutiliwa mkazo na
mbinu za kifani zilizoteuliwa na mwandishi na kwa kufanya hivyo ujumi huimarika,kazi hupata
mvuto na hatimaye maudhui hueleweka vyema na kwa ukamilifu.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: