Usawiri Wa Watoto Katlka Hadithi Za Mwepesi Wa Kusaha Unalikizo Ya Mkosi
View/ Open
Date
2015Author
Miricho, Erastus M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Mada ya utafiti huu ilikuwa kuchunguza usawiri wa watoto katika hadithi za Mwepesi
vva Kusahau na Likizo ya Mkosi. Hadithi hizi za watoto zimejikita katika fasihi ya
watoto. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha taswira za mtoto wa kike na
zile za mtoto wa kiume, kulinganisha sifa za watoto wa kike na wenzao wa kiume na
kuchunguza mitazamo ya watoto wa kike kuhusu wenzao wa kiume katika Mwepesi
lin Kusahau na Likizo ya Mkosi. Nadhariatete mbili zilizoongoza utafiti huu ni
kwamba katika hadithi za watoto msichana huchorwa akiwa mwema kuliko mvulana
na pili ni kuwa wasichana na wavulana katika jamii ya sasa wanajiona kuwa sawa.
Nadharia ya sosholojia ya fasihi iliyotumiwa katika utafiti huu ilitoa msingi
madhubuti wa kutathiminia usawiri wa watoto wa kike na wale wa kiume kwa vile
imethibitika kuwa usawiri unaobainika unafungamana na hali ilivyo katika maisha ya
jamii ya kame hii ya ishirini na moja ambapo inadaiwa wasichana wanaendelea
kuwapiku wavulana katika nyanja mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu na maadili.
Matokeo ya utafiti huu yamethibitisha kuwa katika jamii ya mwandishi mtoto wa kike
anasawiriwa kwa njia chanya zaidi kuliko mtoto wa kiume. Rata hivyo, imedhihirika
kuwa watoto wenyewe hawachukiani baina ya wale wa kike na wale wa kiume.
Kupitia kwa utafiti huu nadhariatete zote mbili zilithibitishwa kuwa kweli. Msichana
amechorwa kama aliye mwema kuliko mvulana. Imethibitishwa pia kuwa katika
kame ya ishirini na moja hakuna majukumu wanayotengewa wasichana ama
wavulana pekee bali wavulana na wasichana wanashirikiana kufanya kazi zozote.
Mapendekezo yametolewa kuwa kuna haja ya kuchukua hatua za dharma
kushughulikia maslahi ya mtoto wa kiume katika jamii. Jambo hili litamwokoa
kutokana na hatari ya kubaki nyuma ya mtoto wa kike katika elimu na shughuli
nyingine za kijamii. Mwishowe, tumetoa mapendekezo ya utafiti zaidi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: