Show simple item record

dc.contributor.authorKariithi, Francis M
dc.date.accessioned2021-09-13T08:10:23Z
dc.date.available2021-09-13T08:10:23Z
dc.date.issued2010
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155465
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kutambulisha mikakati ya upole ya lugha inayotumiwa na vijana katika matumizi yao ya lugha. Vijana wamechukuliwa kama kundi lisilokuwa na hadhari pale linapoitumia lugha katika mazungumzo yanayozungukia miktadha mbalimbali kama vile ya kifo, magonjwa, kazi mbalimbali za sehemu za mwili, maswala ya kujamiiana na kadhalika. Japo kumekuwa na manung'uniko kuhusiana na matumizi ya lugha ya vijana yasiyokuwa na upole, utafiti wetu ulitarajia kuchanganua matumizi safidi ya lugha katika lugha ya rnazungurnzo ya vijana na kuthibitisha kuwa kuna upole unaoendana na matumizi ya lugha kwa vijana kwani wanapoitumia mikakati fulanifulani ili kuzuia kumkirihi mtu katika matumizi yao ya lugha, bila shaka huku ni kudhihirisha kuwepo kwa upole. Ukusanyaji wa data ulifanywa kwa njia ya matumizi ya hojaji ambayo iliyafumbata maswala ambayo kwa kawaida hupelekea mtumiaji wa lugha kuonekana kana kwamba ni mtu aliyepujukwa na maadili ikiwa ataitumia lugha yake kinyume na matarajio ya jamii. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987). IIi kuthibitisha kuwepo kwa mikakati ya upole ya matumizi ya lugha ya vijana, tuliongozwa na matokeo ya namna watafitiwa walivyokuwa wakiangazia maswala tofauti tofauti kwenye hojaji. Tuliwateua vjana 30 kutoka kwa shule tatu za manispaa ya mji wa Nakuru ambapo wavulana walikuwa 15 nao wasichana idadi kama hiyo. Matokeo ya uchanganuzi, 11 yalibainisha bayana kuwa vijana hutumia mseto wa mikakati ya upole katika matumizi yao ya lugha. Ushahidi ulio na mashiko ni kuwa mikakati hutegernea vijana wanawasiliana na nani, mada ni gani na sababu za kuwasiliana ni gani.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMikakati Ya Upole Ya Lugha Katika Matumizi Ya Lugha Ya Vijana'en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States