Mikakati Ya Upole Ya Lugha Katika Matumizi Ya Lugha Ya Vijana'
View/ Open
Date
2010Author
Kariithi, Francis M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulilenga kutambulisha mikakati ya upole ya lugha inayotumiwa na vijana katika
matumizi yao ya lugha. Vijana wamechukuliwa kama kundi lisilokuwa na hadhari pale
linapoitumia lugha katika mazungumzo yanayozungukia miktadha mbalimbali kama vile ya
kifo, magonjwa, kazi mbalimbali za sehemu za mwili, maswala ya kujamiiana na kadhalika.
Japo kumekuwa na manung'uniko kuhusiana na matumizi ya lugha ya vijana yasiyokuwa na
upole, utafiti wetu ulitarajia kuchanganua matumizi safidi ya lugha katika lugha ya
rnazungurnzo ya vijana na kuthibitisha kuwa kuna upole unaoendana na matumizi ya lugha
kwa vijana kwani wanapoitumia mikakati fulanifulani ili kuzuia kumkirihi mtu katika
matumizi yao ya lugha, bila shaka huku ni kudhihirisha kuwepo kwa upole.
Ukusanyaji wa data ulifanywa kwa njia ya matumizi ya hojaji ambayo iliyafumbata maswala
ambayo kwa kawaida hupelekea mtumiaji wa lugha kuonekana kana kwamba ni mtu
aliyepujukwa na maadili ikiwa ataitumia lugha yake kinyume na matarajio ya jamii.
Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia nadharia ya Upole ya Brown na Levinson
(1987). IIi kuthibitisha kuwepo kwa mikakati ya upole ya matumizi ya lugha ya vijana,
tuliongozwa na matokeo ya namna watafitiwa walivyokuwa wakiangazia maswala tofauti
tofauti kwenye hojaji.
Tuliwateua vjana 30 kutoka kwa shule tatu za manispaa ya mji wa Nakuru ambapo
wavulana walikuwa 15 nao wasichana idadi kama hiyo. Matokeo ya uchanganuzi,
11
yalibainisha bayana kuwa vijana hutumia mseto wa mikakati ya upole katika matumizi yao
ya lugha. Ushahidi ulio na mashiko ni kuwa mikakati hutegernea vijana wanawasiliana na
nani, mada ni gani na sababu za kuwasiliana ni gani.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: