Mifichamo Katlka Mashairi Ya Mrisho Mpoto: Nikipata Nauli Sizonje
View/ Open
Date
2018Author
Daniel, Nyamboga,
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulipania kuchunguza mifichamo katika mashiri mawili teule ya Mrisho Mpoto ya
Nikipata Nauli na Sizonje. Kwa kutumia maoni ya Grice (1975) kuhusu kanuni za utaratibu wa
ushirikiano wa kimazungumzo tuliaangaliajinsi ukiukaji wa kanuni za ukweli, idadi, uhusiano na
namna unavyozua mifichamo katika kauli. Tulichunguza mashairi hayo teule ili kutambua kauli
zinazokiuka kanuni za utaratibu wa ushirikiano wa kimazungumzo na kuhakiki mifichamo
inayojitokeza kwa msikilizaji kutokana na ukiukaji wa kanuni hizo. Aidha tulionyesha namna
mfichamo huo unavyochangia katika kukuza maudhui mbali mbali katika mashairi haya mawili.
Utafiti huu, unapendekeza kutumia mtazamo wa kipramatiki-mitindo, wa kuhakiki kazi za kisanaa
katika kuonyesha namna mtindo wa matumizi ya lugha wa Mrisho Mpoto ulivyochangia katika
kuleta ukiukaji wa kanuni katika kauli zake. Aidha tuliangalia mchango wa mkutadha katika
ufasiri wa maana za kazi za kifasihi. Kwa kufanya hivyo tuliona namna kanuni au maarifa ya
kipragmatiki yalivyotumika kueleza maana katika kazi ya kisanaa, hasa ushairi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: