Uchambuzi Wa Tamathali Za Usemi Pamoja Na Mbinu Nyingine Za Matumizi Ya Lugha Katika Utenzi Wa Mikidadi Na Mayasa
Abstract
Utafiti huu unahusu uchambuzi wa tamathali za usemi na mbinu nyengine za
matumizi ya lugha katika Utenzi wa Mikidadi na Mayasa na Said Abdalla Masudi
el Buhry el Hinawy.
Kazi hii imegawanywa katika sura nne. Katika sura ya kwanza tumeelezea swala
letu la utafiti, madhumuni ya utafiti na nadharia tete zinazotuongoza. Isitoshe
tumeeleza sababu za kuchagua mada hii pamoja na kufafanua upeo na mipaka ya
somo hili, yaani utafiti wetu. Pia tumefafanua msingi wa kinadharia wa utafiti
pamoja na yaliyoandikwa kuhusu somo hili, mbinu za utafiti na uchanganuzi wa
data.
Katika sura ya pili tulitanguliza kwa kueleza maana ya fani pamoja ,',:1 kuvitolea
maelezo vipengele mbalimbal i vya fani kikiwemo kipengele cha tamathali za
usemi na mbinu nyingine za matumizi ya Iugha.Tumewarejelea wataalamu mbalimbali
katika kurejelea vipengele hivyo.
Sura ya tatu tumebainisha tamathali tofauti tofauti za usemi pamoja nambinu
nyingine za matumizi ya lugha zilizotumika katika utenzi huu na kuzitolea maelezo
yake. Sura ya nne ni hitimisho.Tumeeleza tuliyoyatambua na kutoa mapendekezo
ya utafiti zaidi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: