Show simple item record

dc.contributor.authorOwino, Martha A
dc.date.accessioned2021-09-16T08:10:11Z
dc.date.available2021-09-16T08:10:11Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155477
dc.description.abstractUtafiti huu ulishughulikia uchanganuzi wa matini teule ya nyimbo za Foustine Munishimtazamo wa nadharia ya upole ya Brown na Levinson (1987) has a kipengele cha mikakati ya kuokoa uso. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha suala la upole katika matini teule ya nyimbo mbili za Foustine Munishi. Foustine Munishi alizingatia upole katika kutunga nyimbo zake tulizoteua. Katika sura ya kwanza, tulieleza kwa ufupi kuhusu usuli wa mada ya utafiti. Tulieleza tatizo la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Katika sura hii pia tulishughulikia sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na njia za utafiti. Tulitumia mbinu ya maktabani katika kukusanya data tuliyohitaji na kuichanganua. Tulithibitisha kuwa kuna mikakati mbalimbali ya kuokoa uso chanya na uso hasi kwenye matini teule ya nyimbo mbili za Munishi. Katika sura ya pili tulishughulikia nyimbo; aina na majukumu kwa jumla na mtindo. Katika sura ya tatu tulibainisha suala la upole katika nyimbo za dini kwa ujumla. Pia tulieleza suala la upole katika matini teule ya wimbo wa Munishi: wimbo wa Maji yana mdudu. Katika sura ya nne tulibainisha suala la upole katika matini teule ya wimbo wa Munishi: wimbo wa Mqlebo. Hitimisho na mapendekezo yametolewa katika sura ya tano.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUchanganuzi Wa Matini Teule Ya Nyimbo Za Foustine Munishi: Mtazamo Wa Nadharia Ya Upoleen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States