Uchanganuzi Wa Matini Teule Ya Nyimbo Za Foustine Munishi: Mtazamo Wa Nadharia Ya Upole
View/ Open
Date
2011Author
Owino, Martha A
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulishughulikia uchanganuzi wa matini teule ya nyimbo za Foustine Munishimtazamo
wa nadharia ya upole ya Brown na Levinson (1987) has a kipengele cha
mikakati ya kuokoa uso.
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha suala la upole katika matini teule ya
nyimbo mbili za Foustine Munishi. Foustine Munishi alizingatia upole katika kutunga
nyimbo zake tulizoteua.
Katika sura ya kwanza, tulieleza kwa ufupi kuhusu usuli wa mada ya utafiti. Tulieleza
tatizo la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Katika sura hii
pia tulishughulikia sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, msingi wa nadharia,
yaliyoandikwa kuhusu mada na njia za utafiti. Tulitumia mbinu ya maktabani katika
kukusanya data tuliyohitaji na kuichanganua. Tulithibitisha kuwa kuna mikakati
mbalimbali ya kuokoa uso chanya na uso hasi kwenye matini teule ya nyimbo mbili za
Munishi.
Katika sura ya pili tulishughulikia nyimbo; aina na majukumu kwa jumla na mtindo.
Katika sura ya tatu tulibainisha suala la upole katika nyimbo za dini kwa ujumla.
Pia tulieleza suala la upole katika matini teule ya wimbo wa Munishi: wimbo wa Maji
yana mdudu. Katika sura ya nne tulibainisha suala la upole katika matini teule ya wimbo
wa Munishi: wimbo wa Mqlebo.
Hitimisho na mapendekezo yametolewa katika sura ya tano.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: