Mchango Wa Vijana Katika Kuleta Mabadiliko Katika Kufa Kuzikana Nakidagaa Kimemwozea
View/ Open
Date
2017Author
Munyasya, Florence M
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Katika utafiti huu, tumeonyesha mchango wa vijana katika kuleta mabadiliko katika riwaya za
Kufa Kuzikana na Kidagaa Kimemwozea. Pia, tumeangazia changamoto ambazo vijana
hukumbana nazo katika juhudi zao za kuleta mabadiliko. Utafiti wetu uliongozwa na nadharia
ya uyakinifu wa kijamii ambao unajihusisha na utetezi wa wanyonge na ukombozi wao.
Tumetambua kwamba vijana ni mawakala wa mabadiliko na wanaweza ku1eta mchango ambao
unaweza kuwafaidi wanajamii wote. Hii ni kwa sababu vijana ni wenye nguvu za mwili na
maarifa ambayo wanaweza kutumia ili kuifunza jamii. Pamoja na haya, tumeonyesha kwamba
vijana wanakabiliana na changamoto nyingi ambazo ni lazima zichukuliwe hatua ili kizazi hiki
ambacho ni muhimu sana kipate kuokolewa. Tulitumia mbinu za utafiti za maktabani na
mtandaoni. Maktabani, tulisoma riwaya mbili teule na makala tofauti kama vile tasnifu na vitabu
vyenye maelezo kuhusu nadharia ya uyakinifu wa kijamii. Tulitembelea mtandao na kuangalia
masuala yanayohusiana na vijana na pia tulisoma maelezo kuhusu nadharia ya uyakinifu wa
kijamii.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [625]
The following license files are associated with this item: