Show simple item record

dc.contributor.authorWarambo, John P
dc.date.accessioned2021-09-16T09:26:26Z
dc.date.available2021-09-16T09:26:26Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155482
dc.description.abstractKatika utafiti huu tulinuia kuchanganua maendeleo ya kisemantiki katika Sheng tukiongozwa na nadharia ya pragmatiki leksika ya Blutner (1990). IIi kufikia malengo hayo, sura ya kwanza imeshughulikia utangulizi kwa ujumla. Katika utangulizi tumezungumzia usuli wa mada, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, haipothesia, msingi wa kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada yetu, njia za utafiti na umuhimu wa utafiti huu. Baada ya utangulizi, tulitambua kwamba leksimu ndizo hubeba maana katika lugha na hivyo kwenye sura ya pili tumezungumzia mbinu za uundaji leksimu. Mbinu zilizoshughulikiwa ni kama; ukopaji na utohozi, ubunifu, uambishaji, uambatishaji, ubadilishaji silabi, taratibu changamano, ukatizaji, onomatopea, akronimu, ujenzi ghairi, uhulutishaji, unyumbuzi kapa, ubadilishaji rajamu na upolisemia. Leksimu baada ya kuundwa hupitia maendeleo ya kisemantiki kwa maana kwamba hubadili maana na hata leksimu kupanuka kimaana; mambo hayo yameshughulikiwa katika sura ya tatu. Hapo ndipo tumebaini mabadiliko ya kisemantiki kama njia mojawapo ya maendeleo ya kisemantiki. Aidha tumebaini michakato ya pragmatiki leksika ikiwa ni kutoa mifano ya data tuliyokusanya nyanjani. IIi kuthibitisha hoja na madai yetu, katika sura ya nne tumeshughulikia ubunifu wa kileksimu. Ubunifu wa leksimu mpya pamoja na ubunifu wa leksimu kupata fahiwa zaidi umejadiliwa. Hapo tumetambua ubunifu wa kileksimu kama mchakato wa pragmatiki leksika huchochewa zaidi na muktadha. Kutokana na matokeo ya uchanganuzi data, ilitubidi kurejelea haipothesia zetu ili kuzikubali. Katika sura ya tano tumetoa muhtasari wa kazi nzima pamoja na kutoa hitimisho na mwishowe kupendekeza sehemu zinazohitaji utafiti zaidi.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUchanganuzi Wa Maendeleo Va Kisemantiki Katika Sheng: Mtazamo Wa Pragmatiki Leksika.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States