Uchanganuzi Wa Maendeleo Va Kisemantiki Katika Sheng: Mtazamo Wa Pragmatiki Leksika.
View/ Open
Date
2011Author
Warambo, John P
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika utafiti huu tulinuia kuchanganua maendeleo ya kisemantiki katika Sheng tukiongozwa
na nadharia ya pragmatiki leksika ya Blutner (1990). IIi kufikia malengo hayo, sura ya
kwanza imeshughulikia utangulizi kwa ujumla. Katika utangulizi tumezungumzia usuli wa
mada, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, haipothesia, msingi wa kinadharia, yaliyoandikwa
kuhusu mada yetu, njia za utafiti na umuhimu wa utafiti huu.
Baada ya utangulizi, tulitambua kwamba leksimu ndizo hubeba maana katika lugha na hivyo
kwenye sura ya pili tumezungumzia mbinu za uundaji leksimu. Mbinu zilizoshughulikiwa ni
kama; ukopaji na utohozi, ubunifu, uambishaji, uambatishaji, ubadilishaji silabi, taratibu
changamano, ukatizaji, onomatopea, akronimu, ujenzi ghairi, uhulutishaji, unyumbuzi kapa,
ubadilishaji rajamu na upolisemia.
Leksimu baada ya kuundwa hupitia maendeleo ya kisemantiki kwa maana kwamba hubadili
maana na hata leksimu kupanuka kimaana; mambo hayo yameshughulikiwa katika sura ya
tatu. Hapo ndipo tumebaini mabadiliko ya kisemantiki kama njia mojawapo ya maendeleo ya
kisemantiki. Aidha tumebaini michakato ya pragmatiki leksika ikiwa ni kutoa mifano ya data
tuliyokusanya nyanjani.
IIi kuthibitisha hoja na madai yetu, katika sura ya nne tumeshughulikia ubunifu wa kileksimu.
Ubunifu wa leksimu mpya pamoja na ubunifu wa leksimu kupata fahiwa zaidi umejadiliwa.
Hapo tumetambua ubunifu wa kileksimu kama mchakato wa pragmatiki leksika huchochewa
zaidi na muktadha.
Kutokana na matokeo ya uchanganuzi data, ilitubidi kurejelea haipothesia zetu ili kuzikubali.
Katika sura ya tano tumetoa muhtasari wa kazi nzima pamoja na kutoa hitimisho na
mwishowe kupendekeza sehemu zinazohitaji utafiti zaidi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: