Show simple item record

dc.contributor.authorMakanga, Miriam A
dc.date.accessioned2021-09-17T06:22:31Z
dc.date.available2021-09-17T06:22:31Z
dc.date.issued2008
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155491
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia uchanganuzi wa kiisimu-matini wa diwani ya Msimu wa Tisa kwa kujikita katika dhana za muala na mshikamano. Uchanganuzi huu umefanywa kwa kufuata mwelekeo wa kinadharia wa muala wa Halliday na Hasan (1976) pamoja na mwelekeo wa umatini na Beaugrande na Dressler (1981). Utafiti huu umegawanywa katika sura nne. Katika sura ya kwanza, tumetanguliza kwa kuelezea juu ya utanzu wa ushairi huru. Tumefafanua pia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, na nadharia tete ambazo zimetumiwa katika utafiti huu. Sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka, na yaliyoandikwa kuhusu mada hii yanajitokeza pia katika sura hii. Aidha, msingi na kinadharia na njia za utafiti zinakamilisha maelezo katika sura hii. Sura ya pili imetafiti muala katika mashairi ya Msimu wa Tisa kwa kuchanganua vipengele vya urejelezi, udondoshaji, ubadilishaji, uunganishaji na muala wa kimsamiati na kuonyesha jinsi vinavyojenga muala. Mwishoni mwa sura hii, tumechora majedwali yanayoonyesha vipashio mbalimbali vya muala katika mashairi ya Msimu wa Tisa. Katika sura ya tatu, tumeanisha vipengele vya 'mshikamano kama vile: mpangilio wa sauti, maneno, sentensi, uhusiano wa mada, anwani na yaliyomo pamoja na muktadha na mandhari ili kubainisha namna vinavyojenga mshikamano katika mashairi ya Msimu wa Tisa. VI Sura ya nne ni hitimisho na mapendekezo ambapo tumehitimisha kwa kueleza viwango vya matumizi ya aina mbalimbali za muala. Matumizi ya vipengele vya mshikamano pia yametolewa. Hatimaye, tumemalizia utafiti huu kwa kutoa mapendekezo ya tafiti za kufanywa na tahakiki za baadaye.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUchanganuzi Wakiisimuen_US
dc.titleUchanganuzi Wakiisimu -matini wamsimuwa Tisaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States