Mwingiliano Wa Fasihi Na Historia Katika Utenzi Wa Nchuu Cwavo Yapo Tini Mwairara (Mtu Ni Kwao Japo Chini Mwa Irara)
Abstract
Tasnifu hii inahusu mwingiliano wa fasihi na historia katika Utenzi wa Nchuu Cwavo
Yapo Tini lvfwa Irara wa Abubaker M.B. Khuchi. Kazi hii ilikuwa na maIengo
mahususi matatu; kwanza, kuhakiki mchango wa historia katika kufumbata dhamira
ya mwandishi wa Utenzi wa Nchuu Cwavo Yapo Tini Mwa Irara. Pili, kuchanganua
kwa kina maudhui kama kipengeIe cha fasihi katika Utenzi wa Nchuu Cwavo Yapo
Tini Mwa Irara na mwisho kutathmini mchango wa mandhari katika Utenzi wa
Nchuu Cwavo Yapo Tini Mwa frara. Tuliongozwa na nadharia ya uhaIisia wa kijamaa
katika kuchanganua kazi hii. Tumefanya uchanganuzi wa maudhui kama kipenge\e
cha fasihi kwa kina. Aidha, tumechanganua mchango wa mandhari katika Utenzi wa
Nchuu Cwavo Yapo Tini Mwa frara na kubaini kuwa kazi hii imejengwa katika
mandhari halisi inayofahamika na wanajamii. VileviIe, tumechunguza jinsi historia na
fasihi zinavyoingiliana na kutegemeana kwa ujumla kabla va kujibu swali letu Ia
utafiti la mwingiliano wa fasihi na historia katika Utenzi wa Nchuu Cwavo Yapo Tini
Mwa lrara. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa mtunzi wa Utenzi wa Nchuu
Cwavo Yapo Tini Mwa frara ameathiriwa na historia ya jamii yake kwa kiwango
kikubwa.
v
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [606]
The following license files are associated with this item: