Abstract
Utafiti huu una lengo la kuweka wazi usayansi uliopo katika istilahi zilizotoholewa kutoka
Kiswahili hadi Ekegusii. Utafiti huu umetumia nadharia ya ukopaji uhamisho na N.I.K. katika
ufafanuzi wa kazi hii. Vile vile uasilia wa istilahi tohozi umechunguzwa iwapo maneno tohozi
yote yalikuwa na majina asilia. Tumegundua kuwa majina asilia mengi yanazidi kufifia kwa
kuwa watumizi wa nomino hizo ni wachache. Mofolojia ya Kiswahili na ya Ekegusii
imelinganishwa. Ukosefu wa fonimu fulani katika lugha moja ndio husababisha tofauti katika
maendelezi. Tofauti kati ya lugha hizi mbili ulibainishwa ingawa zote ni lugha za nasaba moja.
Taratibu za utohozi zimechunguzwa, matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa utohozi huongozwa
na kudhibitiwa na sheri a na kanuni za fonolojia ya Ekegusii.