Show simple item record

dc.contributor.authorOwala, Jael A
dc.date.accessioned2021-09-28T05:27:06Z
dc.date.available2021-09-28T05:27:06Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155526
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, tumechunguza mitazamo kuhusu Kiswahili miongoni mwa wazungurnzaji wa Kijaluo kwa kurejelea shule za msingi katika Kaunti ya Migori. Madhumuni ya utafiti ni, kupambanua mitazamo kuhusu lugha ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, walimu na wazazi wenye asili ya Kijaluo katika Kaunti ya Migori, kuchunguza mambo ambayo husababisha mitazamo tofauti tofauti katika Kaunti ya Migori miongoni mwa wanafunzi, walimu na wazazi kuhusiana na lugha ya Kiswahili na kuchunguza iwapo mitazamo hii ina athari katika matokeo ya mitihani ya Kitaifa ya darasa la nane katika somo la Kiswahili, katika Kaunti ya Migori. Mbinu tulizozitumia katika utafiti ni uchunguzi stahilifu na uchunguzi kiasi. Vilevile tulitumia hojaji, uchunguzi uelekezi pamoja na mahojiano. Maswali yaliyotumiwa katika hojaji yalikuwa maswali ya wazi, maswali funge na maswali ya viwango. Wanafunzi, walimu na wazazi walihojiwa ili kupambanua mitazamo yao katika lugha hii ya Kiswahili. Data ilichanganuliwa kwa kutumia baa grafu, majedwali ya frikwenzi pamoja na pai chati. Nadharia iliyotumiwa ilikuwa nadharia ya Saikolojia ya jamii. Matokeo ya utafiti yalikuwa kwamba, wanafunzi hufurika madarasani kwa hivyo hawashughulikiwi kwa njia inayofaa, walimu wana masomo mengi kupita kiasi kwa hivyo wamekosa motisha, watafitiwa wameathiriwa na lugha nyingine kama vile Kijaluo na Kiingereza. Mapendekezo yalikuwa kwamba, vifaa vya kufunzia na kujifunza kwa lughayaKiswahili viwe vya kutosha, walimu wa Kiswahili wanapaswa kuhudhuria warsha na kozi za kunoa ubongo, sera za shule kuhusu lugha zitumike kwa usawa, mandhari ya shule yasionyeshe mapendeleo, maingiliano kuhusu lugha ya Kiswahili yaimarishwe na mwisho Kiswahili kipewe hadhi kubwa kuliko lugha nyingine kama vile Kijaluo katika Kaunti ya Migori.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMitazamo Kuhusu Kiswahili Miongoni Mwa Wazungumzaji Wa Kijaluo- Kifani Cha Shule Za Msingi Katika Kaunti Ya Migori.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States