Mitazamo Kuhusu Kiswahili Miongoni Mwa Wazungumzaji Wa Kijaluo- Kifani Cha Shule Za Msingi Katika Kaunti Ya Migori.
Abstract
Katika tasnifu hii, tumechunguza mitazamo kuhusu Kiswahili miongoni mwa
wazungurnzaji wa Kijaluo kwa kurejelea shule za msingi katika Kaunti ya Migori.
Madhumuni ya utafiti ni, kupambanua mitazamo kuhusu lugha ya Kiswahili miongoni
mwa wanafunzi, walimu na wazazi wenye asili ya Kijaluo katika Kaunti ya Migori,
kuchunguza mambo ambayo husababisha mitazamo tofauti tofauti katika Kaunti ya
Migori miongoni mwa wanafunzi, walimu na wazazi kuhusiana na lugha ya Kiswahili na
kuchunguza iwapo mitazamo hii ina athari katika matokeo ya mitihani ya Kitaifa ya
darasa la nane katika somo la Kiswahili, katika Kaunti ya Migori. Mbinu tulizozitumia
katika utafiti ni uchunguzi stahilifu na uchunguzi kiasi. Vilevile tulitumia hojaji,
uchunguzi uelekezi pamoja na mahojiano. Maswali yaliyotumiwa katika hojaji yalikuwa
maswali ya wazi, maswali funge na maswali ya viwango. Wanafunzi, walimu na wazazi
walihojiwa ili kupambanua mitazamo yao katika lugha hii ya Kiswahili. Data
ilichanganuliwa kwa kutumia baa grafu, majedwali ya frikwenzi pamoja na pai chati.
Nadharia iliyotumiwa ilikuwa nadharia ya Saikolojia ya jamii. Matokeo ya utafiti
yalikuwa kwamba, wanafunzi hufurika madarasani kwa hivyo hawashughulikiwi kwa
njia inayofaa, walimu wana masomo mengi kupita kiasi kwa hivyo wamekosa motisha,
watafitiwa wameathiriwa na lugha nyingine kama vile Kijaluo na Kiingereza.
Mapendekezo yalikuwa kwamba, vifaa vya kufunzia na kujifunza kwa lughayaKiswahili
viwe vya kutosha, walimu wa Kiswahili wanapaswa kuhudhuria warsha na kozi za kunoa
ubongo, sera za shule kuhusu lugha zitumike kwa usawa, mandhari ya shule yasionyeshe
mapendeleo, maingiliano kuhusu lugha ya Kiswahili yaimarishwe na mwisho Kiswahili
kipewe hadhi kubwa kuliko lugha nyingine kama vile Kijaluo katika Kaunti ya Migori.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [754]
The following license files are associated with this item: