Show simple item record

dc.contributor.authorGaithuma, Virginia W
dc.date.accessioned2021-09-28T05:34:03Z
dc.date.available2021-09-28T05:34:03Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155527
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu uchanganuzi wa athari za kifonolojia za lahaja za Kiamu na Kitikuu katika Kiswahili sanifu ambapo uchanganuzi huu unahusu kulinganisha miundo mbalimbali ya maneno katika insha za wanafunzi na kuonyesha tofauti zinazojitokeza katika maneno kutokana na lahaja za Kiamu na Kitikuu katika Kiswahili sanifu. Uchunguzi huu ulinuia kubainisha fonimu za lahaja ya Kiamu na Kitikuu, kuonyesha athari za kisauti katika Kiswahili sanifu kutokana na lahaja za Kiamu na Kitikuu katika kazi andishi za wanafunzi na pia kuorodhesha fonimu za Kiswahili sanifu. Utafiti huu umetumia nadharia ya Lugha Kati hasa kwa kurejelea mifanyiko mitano ya kisaikolojia kama mihimili mikuu. Nadharia ya Lugha Kati ilitumiwa kueleza ni vipi lugha kati huzalika miongoni mwa wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Kiamu au Kitikuu wanapojifundisha Kiswahili sanifu. Lugha wanayoizungumza baada ya juhudi za kujifunza sio Kiswahili sanifu bali ni lugha iliyo kati ya lahaja ya Kiamu na Kitikuu na Kiswahili sanifu ambayo ndio huitwa lugha kati. Utafiti huu ulitumia mbinu ya uteuzi wa sampuli ambapo wanafunzi arobaini wa darasa la saba kutoka shule one tofauti za kimsingi katika kisiwa cha Lamu waliteuliwa na insha walizoziandika kuchunguzwa. Matokeo ya utafiti katika tasnifu hii yanadhihirisha kwamba lahaja ya Kiamu ina fonimu 35 na lahaja ya Kitikuu ina fonimu 34. Vilevile ilidhihirika kwamba kulikuwa na athari mbalimbali za kisauti katika Kiswahili sanifu kutokana na lahaja za Kiamu na Kitikuu ambapo athari ya matumizi ya Ij/ badala ya 1]1 ilionekana kuenea sana miongoni mwa wanafunzi tuliowachunguza ambao lugha yao ya kwanza ni aidha lahaja ya Kiamu au Kitikuu. Utafiti huu vilevile ulibainisha kwamba lahaja ya Kitikuu ilikuwa na athari nyingi za kisauti na zilizo tofauti katika Kiswahili sanifu ikilinganishwa na lahaja ya Kiamu. Mwisho ilibainika kwamba lugha iliyozungumzwa na wanafunzi tuliowachunguza ambao lugha yao ya kwanza ni aidha lahaja ya Kiamu au Kitikuu wanapojifundisha Kiswahili sanifu ni lugha kati kwani lugha hiyo haikufikia kiwango cha kuitwa Kiswahili sanifu kutokana na athari mbalimbali tulizozitambua miongoni mwa wanafunzi tuliowachunguza.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleAthari Za Kifonolojia Za Lahaja Ya Kiamu Na Kitikuu Katika Kiswahili Sanifuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States