Athari Za Kifonolojia Za Lahaja Ya Kiamu Na Kitikuu Katika Kiswahili Sanifu
View/ Open
Date
2016Author
Gaithuma, Virginia W
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii inahusu uchanganuzi wa athari za kifonolojia za lahaja za Kiamu na Kitikuu katika
Kiswahili sanifu ambapo uchanganuzi huu unahusu kulinganisha miundo mbalimbali ya maneno
katika insha za wanafunzi na kuonyesha tofauti zinazojitokeza katika maneno kutokana na lahaja
za Kiamu na Kitikuu katika Kiswahili sanifu. Uchunguzi huu ulinuia kubainisha fonimu za
lahaja ya Kiamu na Kitikuu, kuonyesha athari za kisauti katika Kiswahili sanifu kutokana na
lahaja za Kiamu na Kitikuu katika kazi andishi za wanafunzi na pia kuorodhesha fonimu za
Kiswahili sanifu. Utafiti huu umetumia nadharia ya Lugha Kati hasa kwa kurejelea mifanyiko
mitano ya kisaikolojia kama mihimili mikuu. Nadharia ya Lugha Kati ilitumiwa kueleza ni vipi
lugha kati huzalika miongoni mwa wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Kiamu au Kitikuu
wanapojifundisha Kiswahili sanifu. Lugha wanayoizungumza baada ya juhudi za kujifunza sio
Kiswahili sanifu bali ni lugha iliyo kati ya lahaja ya Kiamu na Kitikuu na Kiswahili sanifu
ambayo ndio huitwa lugha kati. Utafiti huu ulitumia mbinu ya uteuzi wa sampuli ambapo
wanafunzi arobaini wa darasa la saba kutoka shule one tofauti za kimsingi katika kisiwa cha
Lamu waliteuliwa na insha walizoziandika kuchunguzwa. Matokeo ya utafiti katika tasnifu hii
yanadhihirisha kwamba lahaja ya Kiamu ina fonimu 35 na lahaja ya Kitikuu ina fonimu 34.
Vilevile ilidhihirika kwamba kulikuwa na athari mbalimbali za kisauti katika Kiswahili sanifu
kutokana na lahaja za Kiamu na Kitikuu ambapo athari ya matumizi ya Ij/ badala ya 1]1
ilionekana kuenea sana miongoni mwa wanafunzi tuliowachunguza ambao lugha yao ya kwanza
ni aidha lahaja ya Kiamu au Kitikuu. Utafiti huu vilevile ulibainisha kwamba lahaja ya Kitikuu
ilikuwa na athari nyingi za kisauti na zilizo tofauti katika Kiswahili sanifu ikilinganishwa na
lahaja ya Kiamu. Mwisho ilibainika kwamba lugha iliyozungumzwa na wanafunzi
tuliowachunguza ambao lugha yao ya kwanza ni aidha lahaja ya Kiamu au Kitikuu
wanapojifundisha Kiswahili sanifu ni lugha kati kwani lugha hiyo haikufikia kiwango cha kuitwa
Kiswahili sanifu kutokana na athari mbalimbali tulizozitambua miongoni mwa wanafunzi
tuliowachunguza.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [606]
The following license files are associated with this item: