Show simple item record

dc.contributor.authorOkombo, Patrick L
dc.date.accessioned2021-10-13T09:54:45Z
dc.date.available2021-10-13T09:54:45Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155604
dc.description.abstractUtenzi wa Tambuka ni miongoni mwa tenzi ndefu na za jadi za Kiswahili. Utenzi huu wenye beti 1150 unahusu tukio la vita baina ya Waislamu na Wakristo katika mji wa Tambuka vikiongozwa na Mtume Muhammadi na mfalme Herekali mtawalia. Utenzi huu ulitungwa na Bwana Athumani bin Mwengo katika mwaka wa 1728. Utafiti huu ulihusu uhakiki wa kimtindo wa Utenzi wa Tambuka. Kipengele cha kimtindo kilichoshughulikiwa ni tamathali za usemi hususan sitiari, taashira na tashibiha. Utafiti ulichunguza mchango wa tamathali hizi katika uwasilishaji wa dhamira ya Utenzi wa Tambuka. Utafiti ulilenga kudhihirisha kuwa Utenzi wa Tambuka una ukwasi wa sitiari, taashira na tashibiha na kwamba tamathali hizi ndizo mihimili ya dhamira ya utenzi huu. Tumeigawa tasnifu hii katika sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi. Imeshughulikia maswala ya kimsingi ya utafiti huu. Maswala haya ni pamoja na tatizo Ia utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada na upeo na mipaka ya utafiti. Aidha, tumeelezea misingi ya kinadharia, tukadurusu yaliyoandikwa kuhusu somo hili na vilevile tukaelezea mbinu za utafiti. Sura ya pili inahusu ufafanuzi wamisingi ya kinadharia ya sitiari, taashira ta tashibiha. Tumezijadili tamathali hizi kwa undani, kuziainisha na kutolea mifano ili kuweka wazi maelezo yake. Ni katika sura hii ndipo tunaonyesha kuwa sitiari, taashira na tashibiha ni tamathali za usemi zenye uhusiano wa karibu unaotokana na sababu kuwa zote zinahusu mlinganisho wa hulka. Sura ya tatu inahusu uhakiki wa matumizi ya sitiari katika Utenzi wa Tambuka. Msisitizo wetu uko kwenye uamili wa sitiari katika uwasilishaji wa dhamira ya Utenzi wa Tambuka. Hata hivyo, xii turnegusia kuhusu dhima nyinginezo za kiumbuji za sitiari katika utenzi huu. Ni katika surahii ndipo tunaonyesha kuwa sitiari zinazojitokeza katika Utenzi wa Tambuka zinaweza kuainishwa kwa rnisingi ya vilinganishi vyake. Vilinganishi vyenyewe ni pamoja na wanyama, vitu vya kiasiliana vifaa au vyombo mbalimbali. Katika sura ya nne, tunahakiki matumizi ya taashira na aina zake maalum katika uwasilishaji wa dharnira ya Utenzi wa Tambuka. Utafiti unaonyesha kwamba aina maalum za taashira zinazojitokeza katika Utenzi wa Tambuka ni sinekidoki na lakabu. Taashira na sinekidoki zinazotumiwa hasa zinahusu matumizi ya sehemu fulani za mwili wa binadamu kusimamia aidha rnwilirnzima au jambo fulani kuhusu maisha ya mtu. Hali kadhalika, sura hii inaonyesha kuwa lakabuzinazotumiwa kuwarejelea Mungu, Muhammadi na Ali ni nyingi na chanya. Herekeli na Wakristo wenzake hawajarejelewa kwa lakabu nyingi. Lakabu ya pekee inayojitokeza ni 'Kufari', ambayo ni hasi mno. Sura ya tano inachunguza matumizi ya tashibiha katika uwasilishaji wa dhamira ya Utenzi wa Tambuka. Tashibiha zinazojitokeza katika utenzi huu zinaainishwa kwa misingi ya vilinganishi vilivyotumiwa. Vilinganishi hivi ni wanyama, wadudu, samaki, viumbe dhahania, hali, maji na vyanzo vyake na moto. Utafiti unabainisha kwamba wahusika Waislamu wamelinganishwa na vitu hatari au vyenye maangamizo makuu. Kwa upande mwingine, wahusika Wakristo wanalinganishwa na vitu vinavyodhaniwa kuwa 'dhaifu' na 'potofu'. Sura ya sita inahusu hitimisho la utafiti. Katika sehemu hii, tunarejelea mada ya utafiti huu na rnaswala mengine ya kimsingi tuliyoyaelezea katika sura ya kwanza. Aidha, tunapima nadharia tete za utafiti huu, ambapo tunaonyesha kuwa Utenzi wa Tambuka una ukwasi wa sitiari, taashira na tashibiha na kuwa tamathali hizi ni mihimili ya dhamira ya utenzi huu. Hatimaye, tunatoa xiii mapendekezo kuwa utafiti zaidi ufanywe kuhusu vipengele vingine vya kimtindo vinavyotumika katika utenzi huu. Vilevile, tunapendekeza kuwa utafiti zaidi ufanywe kuhusu Utenzi wa Tambukakwa kutumia nadharia tofauti na tuliyotumia katika uhakiki huu. Baada ya sura ya sita, tunatoa marejeleo muhimu pamoja na kiambatisho cha nakala ya muswada wa Utenziwa Tambuka tulioutumia katika utafiti huu.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectTashibiha Katika Uwasilishaji Wa Dhamiraen_US
dc.titleSitiari, Taashira Na Tashibiha Katika Uwasilishaji Wa Dhamira Katika Utenzi Wa Tambuka: Uhakiki Wa Kimtindoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States