Sitiari, Taashira Na Tashibiha Katika Uwasilishaji Wa Dhamira Katika Utenzi Wa Tambuka: Uhakiki Wa Kimtindo
View/ Open
Date
2011Author
Okombo, Patrick L
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utenzi wa Tambuka ni miongoni mwa tenzi ndefu na za jadi za Kiswahili. Utenzi huu wenye beti
1150 unahusu tukio la vita baina ya Waislamu na Wakristo katika mji wa Tambuka vikiongozwa
na Mtume Muhammadi na mfalme Herekali mtawalia. Utenzi huu ulitungwa na Bwana
Athumani bin Mwengo katika mwaka wa 1728.
Utafiti huu ulihusu uhakiki wa kimtindo wa Utenzi wa Tambuka. Kipengele cha kimtindo
kilichoshughulikiwa ni tamathali za usemi hususan sitiari, taashira na tashibiha. Utafiti
ulichunguza mchango wa tamathali hizi katika uwasilishaji wa dhamira ya Utenzi wa Tambuka.
Utafiti ulilenga kudhihirisha kuwa Utenzi wa Tambuka una ukwasi wa sitiari, taashira na
tashibiha na kwamba tamathali hizi ndizo mihimili ya dhamira ya utenzi huu.
Tumeigawa tasnifu hii katika sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi. Imeshughulikia maswala
ya kimsingi ya utafiti huu. Maswala haya ni pamoja na tatizo Ia utafiti, madhumuni ya utafiti,
nadharia tete, sababu za kuchagua mada na upeo na mipaka ya utafiti. Aidha, tumeelezea misingi
ya kinadharia, tukadurusu yaliyoandikwa kuhusu somo hili na vilevile tukaelezea mbinu za
utafiti.
Sura ya pili inahusu ufafanuzi wamisingi ya kinadharia ya sitiari, taashira ta tashibiha.
Tumezijadili tamathali hizi kwa undani, kuziainisha na kutolea mifano ili kuweka wazi maelezo
yake. Ni katika sura hii ndipo tunaonyesha kuwa sitiari, taashira na tashibiha ni tamathali za
usemi zenye uhusiano wa karibu unaotokana na sababu kuwa zote zinahusu mlinganisho wa
hulka.
Sura ya tatu inahusu uhakiki wa matumizi ya sitiari katika Utenzi wa Tambuka. Msisitizo wetu
uko kwenye uamili wa sitiari katika uwasilishaji wa dhamira ya Utenzi wa Tambuka. Hata hivyo,
xii
turnegusia kuhusu dhima nyinginezo za kiumbuji za sitiari katika utenzi huu. Ni katika surahii
ndipo tunaonyesha kuwa sitiari zinazojitokeza katika Utenzi wa Tambuka zinaweza kuainishwa
kwa rnisingi ya vilinganishi vyake. Vilinganishi vyenyewe ni pamoja na wanyama, vitu vya
kiasiliana vifaa au vyombo mbalimbali.
Katika sura ya nne, tunahakiki matumizi ya taashira na aina zake maalum katika uwasilishaji wa
dharnira ya Utenzi wa Tambuka. Utafiti unaonyesha kwamba aina maalum za taashira
zinazojitokeza katika Utenzi wa Tambuka ni sinekidoki na lakabu. Taashira na sinekidoki
zinazotumiwa hasa zinahusu matumizi ya sehemu fulani za mwili wa binadamu kusimamia aidha
rnwilirnzima au jambo fulani kuhusu maisha ya mtu. Hali kadhalika, sura hii inaonyesha kuwa
lakabuzinazotumiwa kuwarejelea Mungu, Muhammadi na Ali ni nyingi na chanya. Herekeli na
Wakristo wenzake hawajarejelewa kwa lakabu nyingi. Lakabu ya pekee inayojitokeza ni
'Kufari', ambayo ni hasi mno.
Sura ya tano inachunguza matumizi ya tashibiha katika uwasilishaji wa dhamira ya Utenzi wa
Tambuka. Tashibiha zinazojitokeza katika utenzi huu zinaainishwa kwa misingi ya vilinganishi
vilivyotumiwa. Vilinganishi hivi ni wanyama, wadudu, samaki, viumbe dhahania, hali, maji na
vyanzo vyake na moto. Utafiti unabainisha kwamba wahusika Waislamu wamelinganishwa na
vitu hatari au vyenye maangamizo makuu. Kwa upande mwingine, wahusika Wakristo
wanalinganishwa na vitu vinavyodhaniwa kuwa 'dhaifu' na 'potofu'.
Sura ya sita inahusu hitimisho la utafiti. Katika sehemu hii, tunarejelea mada ya utafiti huu na
rnaswala mengine ya kimsingi tuliyoyaelezea katika sura ya kwanza. Aidha, tunapima nadharia
tete za utafiti huu, ambapo tunaonyesha kuwa Utenzi wa Tambuka una ukwasi wa sitiari, taashira
na tashibiha na kuwa tamathali hizi ni mihimili ya dhamira ya utenzi huu. Hatimaye, tunatoa
xiii
mapendekezo kuwa utafiti zaidi ufanywe kuhusu vipengele vingine vya kimtindo vinavyotumika
katika utenzi huu. Vilevile, tunapendekeza kuwa utafiti zaidi ufanywe kuhusu Utenzi wa
Tambukakwa kutumia nadharia tofauti na tuliyotumia katika uhakiki huu.
Baada ya sura ya sita, tunatoa marejeleo muhimu pamoja na kiambatisho cha nakala ya muswada
wa Utenziwa Tambuka tulioutumia katika utafiti huu.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [754]
The following license files are associated with this item: